Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Licha ya uwepo wa tiba ya tatizo hili, ipo haja ya watu kubadili mfumo wa maisha ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi yatakayochangia meno kutoboka yanayozidi kuenea duniani yakiathiri kila mtu, wakiwamo watoto wadogo.
 
Kutoa taarifa ya maumivu ili kuchunguza meno na kinywa chote ni moja ya namna sahihi za kutambua jino au meno yaliyotoboka ama kuoza. Endapo kutakuwa na haja kwa ushauri wa daktari, mgonjwa anaweza akafanyiwa X-ray. Kila mwenye meno ana uwezekano wa kupata matundu kwenye meno kutokana na sababu tofauti ambayo yasipotibiwa mapema huweza kuathiri matabaka ya jino na kusababisha maumivu makali ambayo yakizidi mgonjwa huweza kuling’oa endapo jitihada za kulitibu hazitafanikiwa.
 
Mara nyingi meno yanayotoboka ni ya nyuma. Yanaitwa magego au masagego. Kwa umbile, yana mifereji ambayo ni rahisi kwa mabaki ya chakula kujishika. Yapo nyuma ukilinganisha na meno mengine hivyo kuongeza ugumu wa kuyasafisha. Wengi hawafikishi mswaki maeneo ya nyuma ya kinywa.
 
Vyakula na vinywaji

Baadhi ya vyakula na vinywaji huweza kujishika kwenye meno kwa muda mrefu. Hivi ni maziwa, ice cream, keki, na mkate hivyo kusababisha meno kutoboka kuliko vinywaji na vyakula ambavyo vinaweza kusafishika na kusafirishwa na mate kiurahisi.
 
Sukari

Unapotumia vinywaji vya sukari mara kwa mara unatoa fursa nzuri kwa bakteria walioko kinywani kushambulia meno yako kwa sababu unatoa fursa ya meno yako kukutana na tindikali muda mwingi ukilinganisha na mtu asiyetumia.
 
Kumlisha mtoto wakati wa kulala

Wazazi wanapaswa kuepuka kuwalisha watoto wadogo vyakula hasa vyenye sukari ili kuwafanya walale kwa sababu vitaendela kuwapo kinywani kwa muda mrefu baada ya mtoto kusinzia hivyo kuozesha meno yake mapema.
 
Kutopiga mswaki

Ingawa inaripotiwa kuwa karibu kila mtu duniani anapiga mswaki, ukweli ni kwamba kuna upungufu kwenye upigaji huo miongoni mwetu. Watu wengi wana haraka kwenye kupiga mswaki hivyo kujikuta hawaufikishi sehemu zote za kinywa.
 
Kutokana na faida yake madini haya huongezwa kwa makusudi kwenye maji ya kunywa kwa viwango stahiki.

Kutokana ukweli huo, unywaji wa maji ya kutosha kila siku, licha ya faida nyinginezo mwilini, huimarisha ubora wa meno.
 
Vilevile dawa za meno huwekwa madini hayo ili kuyaimarisha meno yetu. Ni muhimu kuhakikisha dawa ya meno unayotumia ina madini ya floridi.

Kinywa kikavu

Kinywa kikavu ni matokeo ya upungufu wa mate ambayo kiasili huzuia kutoboka kwa meno kwa kuondoa mabaki ya chakula na utando mlaini kwenye meno.
 
Matibabu

Tiba ya jino siyo kung’oa kama inavyoaminika. Ukweli ni kwamba kung'oa jino kutokana na sababu nyingi za kitabibu ambazo zinajitosheleza kwenye muktadha husika.

Kwenye tasnia ya tiba ya kinywa na meno, kung’oa jino lenye tatizo huwa ni hatua ya mwisho baada ya matibabu mengine kushindikana kutokana na sababu tofauti.
 
Vilevile kemikali zilizomo kwenye mate husaidia kupambana na tindikali izalishwayo na bakteria na kutoboa meno.

Ukavu wa kinywa huweza kuleta vitu vinavyoathiri meno kama vile baadhi ya dawa za kutibu magonjwa mbalimbali, magonjwa yanayoathiri matezi, matibabu ya mionzi ya saratani kichwani au shingoni.

Haya yote huongeza uwezekano wa kutoboka kwa meno kutokana na kupunguza uzalishaji wa mate ambayo ni kinga ya kwanza kuepuka kutoboka.
 
Back
Top Bottom