Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Ningpenda kuona anastahili, lakini katika kipindi cha majira ya joto atarudi nyumbani akiwa ni bingwa.” Aliongeza Guardiola ambaye pia staa wake mwingine, Leroy Sane alichaguliwa kuwa mwanasoka bora chipukizi wa msimu huu. Salah mpaka sasa amefunga mabao 31 na anaongoza kwa kufunga mabao katika Ligi Kuu ya England huku kwa ujumla akiwa amefunga mabao 41 katika michuano mbalimbali ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu anunuliwe na Liverpool akitokea Roma kwa dau la pauni 37 milioni katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto.