Badhi ya miiko ambayo wengi wetu tumekutana nayo kwenye jamii mbalimbali au makabila mbalimbali ni kama hii ifuatayo:
1. Usipige mruzi usiku, utamwita shetani
2. Ukisimulia hadithi mchana, utaota mkia
3. Usikalie Kinu Mwanamke Hutajaaliwa Kuzaa
4. Ukiona zeru zeru Usimzarau au temea mate kifuani
5. Usitoe au kuomba chumvi kwa jirani usiku.
6. Usishone nguo wakati umeivaa, utakua maskini wa kutupwa
7. Usishone chupi iliyochanika