Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Basi kwa kupitia makala hii, tunaweza kuchambua baadhi ya Mila na tamaduni mbalimbali ambazo tunaziona kuwa ni aidha hazikutakiwa kuwepo katika jamii au zilikuwa na lengo aidha kunyanyasa au kumnyanyasa Mwanamke au hata kumshushia hadhi yake. Au tu hazikupaswa kuwepo kutokana na sababu moja au nyingine ambazo msomaji unaweza kuelezea kwa ufupi kwanini unaona kuwa Utamaduni ule, au Mwiko/Miiko ile hakupaswa kufuatwa na jamii husika.
 
Badhi ya miiko ambayo wengi wetu tumekutana nayo kwenye jamii mbalimbali au makabila mbalimbali ni kama hii ifuatayo:

1. Usipige mruzi usiku, utamwita shetani
2. Ukisimulia hadithi mchana, utaota mkia
3. Usikalie Kinu Mwanamke Hutajaaliwa Kuzaa
4. Ukiona zeru zeru Usimzarau au temea mate kifuani
5. Usitoe au kuomba chumvi kwa jirani usiku.
6. Usishone nguo wakati umeivaa, utakua maskini wa kutupwa
7. Usishone chupi iliyochanika
 
8. Mwanamke Mja Mzito haifai kula Mayai (Baadhi ya vyakula), atazaa mtoto Kipara
9. Usimpige mwenzio kwa nguo
10. Usimpige mwenzako kwa fagio
11. Usimruke mwenzako miguu
12. Kufagia Chumba Usiku kunafukuza bahati (Kama iktokea unafagia usiku basi usitupe taka nje, subiri mpaka asubuhi ndio uzitupe)
13. Usitupe Nguo Yako ya Ndani Kitambaa Chochote Chenye Hedhi Mbaya Wako Akitupia Jicho Hutozaa
14. Mwanaume asilie kwenye sufuria la sivyo atakosa mke.
15. Bundi akitua juu ya nyumba yenye mgonjwa na akali, basi kutakuwa na msiba (Mgonjwa atafariki).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…