Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usiharakishe kutuma fedha kwa mtu aliyekutumia ujumbe mfupi wa simu kukutaarifu kwamba mwanao amelazwa hospitalini; ni utapeli mpya unaozidi kusambaa kwa sasa.

Wazazi ndio walengwa wakuu wa utapeli huu wa njia ya simu unaofanywa na watu wanaotafuta taarifa za kutosha kuhusu mwanao kabla ya kukutumia ujumbe huo.
 
Matapeli hao wamekuwa wakiwatumia ujumbe wazazi kuwa watoto wao ni wagonjwa na wamepelekwa hospitali hivyo, kuomba fedha za haraka kusaidia kuharakisha matibabu.

Na ili kukuaminisha, matapeli hao hujifanya ni walimu wa mtoto wako na kutoa taarifa zinazoweza kukuaminisha kwa haraka kuwa kuna tatizo la kweli. Zaidi ya hayo, husisitiza kuwa hali ya ugonjwa wa mtoto wako ni mbaya, hivyo kuhitaji msaada wa fedha ili kuokoa maisha yake.
 
Habari ndugu mimi ni mwalimu, mtoto anaumwa hapa shuleni tuwasiliane haraka,” unasema ujumbe wa tapeli mmoja uliotumwa kwa mzazi ambaye mwanaye anasoma shule moja wilayani Temeke.

Akizungumza na Mwananchi, mzazi huyo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema Aprili 24 saa 5:04 asubuhi alipokea ujumbe huo mfupi wa simu ukimtaarifu kuwa mtoto wake anayesoma kidato cha kwanza, anaumwa.
 
Baada ya kuusoma aliamua kupiga namba iliyomtumia ujumbe huo ili apate taarifa zaidi.

Alisema alipompigia simu mtu huyo alimweleza kuwa mtoto wake anaumwa na hali yake ni mbaya na kwamba wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hivyo afanye awezalo aende hospitalini haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…