Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Timu hizi zinatarajiwa kushuka dimbani Juni 17 pale Rostov Arena kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa kundi hilo. Uwepo wa nyota mbalimbali ambao wanafanya vizuri kwenye soka barani Ulaya kwa sasa, ndio unaongeze utamu wa mchezo baina yao.
 
Kama ilivyo kwa mataifa mengine ambayo yatashiriki fainali za mwaka huu, Brazil na Uswisi, zimeshafahamu mahali ambapo vikosi vyao vitapiga kambi nchini Urusi kwenye fainali hizo. Timu hizo zinatarajiwa kuweka kambi kwenye maeneo yafauatayo
 
Brazil (Swissotel Resort Sochi Camellia, Sochi)

Kikosi hiki kinachomjumuisha mmoja wa mastaa wakubwa wa soka duniani, Neymar, kitaweka kambi Swissotel Resort iliyopo katika mji wa Sochi. Hii ni hoteli ya kitalii iliyojengwa kisasa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kitalii na kibiashara.
 
Hoteli hii ipo kwenye kitovu cha Jiji la Sochi katika eneo la Kurortny Prospekt. Miongoni mwa miundombinu iliyopo kwenye hoteli hii yenye hadhi ya Nyota Tano ni pamoja na bwawa la kuogelea na sehemu ya mazoezi ya viungo (Gym).
 
Uswisi (Togliatti Resort)

Vijana wa Uswisi wao wamechagua kukaa Togliatti Resort iliyopo eneo la Volga, ambapo pana umbali wa kilomita 100 kutoka mji wa Samara ambao ni miongoni mwa miji 11 itakayotumika kwa ajili ya mechi za fainali za mwaka huu.
 
Back
Top Bottom