Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ingawa dalili za mafua sio mbaya sana na hazidumu kwa zaidi ya wiki tatu, utafiti unaonyesha kuwa mafua huchangia kukwamisha maendeleo kwa kiasi fulani. Utafiti uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archival of Internal Medicine, umebaini mafua yanaweza kusababisha mgogoro wa uchumi wa mtu ikiwa ataugua kwa kpindi kirefu na kushindwa kufanya kazi zake za kila siku za kumwingizia kipato.
 
Utafiti huo uliohusisha kaya 4,051 huko Marekani, ulionyesha kuwa takribani dola bilioni 40 za Serikali ya Marekani hupotea kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua (respiratoy diseases) yatokanayo na virusi vya mafua.
 
KISABABISHI CHA MAFUA.

Mafua yanasababishwa na virusi vya aina mbalimbali. Kuna zaidi ya aina 200 ya virusi visababishavyo mafua. Kirusi aina ya ‘’rhinoviruses’’ ndicho kinachosababisha mafua kwa asilimia kubwa 30 hadi 80 ukilinganisha na virusi vya aina nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…