You don't have to be afraid of what may be going on in life or what lies ahead. God is right here with you and will help you get through any situation.
Brighton wanatarajiwa kukoleza ushirikiano na Gereza la Lewes kama sehemu ya mpango wa kuwasaidia wafungwa kuzoea maisha ya kawaida baada ya kuachiliwa huru. (Argus)
Mpenzi wa mchezaji wa zamani wa Newcastle Davide Santon amesema ana wasiwasi kuhusu kukaa kwao nyumbani baada yake na beki huyo wa Inter Milan kutumiwa ujumbe wa vitisho. (Football Italia)
Meneja wa Leicester City Claude Puel amesema pengine wachezaji wameanza kuleweshwa na Kombe la Dunia au mambo mengine baada ya uchezaji wa timu yake kudorora. Walichapwa 5-0 na Crystal Palace. (Guardian)
Wachezaji wa Newcastle hatimaye walipata fursa ya kushiriki sherehe yao ya Krismasi mwishoni mwa wiki. (Newcastle Chronicle)
Mkufunzi mkuu wa Watford Javi Gracia amesema ana imani kikamilifu na watabibu wa timu hiyo licha ya kutokea kwa msururu wa visa vya wachezaji wa klabu hiyo ya Vicarage Road kuumia. (Watford Observer)
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema washambuliaji wake Gareth Bale, 28, na Karim Benzema, 30, "watasalia" katika klabu hiyo licha ya tetesi kudokeza kwamba huenda wakahama. (Star)