Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwa vitu vinavyounda mlo kamili na ulio bora ni pamoja na matunda. Watu wengi wamekuwa na tabia ya kuambatanisha matunda katika milo yao jambo ambalo ni zuri kwa afya.

Embe limekuwa ni miongoni mwa matunda ambayo watu wengi huyatumia mara kwa mara. Hii ni kutokana na utamu wake.
 
Zipo aina mbalimbali za tunda hili kama vile embe dodo, embe ng’ong’o, ‘apple mango, na mengine mengi hapa nchini.

Japokuwa hili ni tunda la msimu, lakini watu wengi hulipenda na hulitumia mara kwa mara, pengine kwa kufahamu umuhimu wake kwa afya ama tu kwa kufurahia utamu wake.
 
Tunda hili ni moja ya matunda muhimu sana kwa afya ya binadamu kwani lina faida nyingi sana. hili ni moja ya matunda machache ambayo yanaupa mwili virutubisho vingi kwa wakati mmoja.

Hizi ni baadhi ya faida utakazozipata ukitumia embe kwa wingi.
 
Huongeza hamu ya kufanya mapenzi na nguvu za kiume

Tunda la embe lina wingi wa Vitamin E ambayo ni kichocheo kikubwa cha kukupa hamu ya kufanya mapenzi. Vile vile lina virutubisho muhimu ambavyo huwasaidia hasa wanaume katika kuimarisha misuli ya uume na kuwaongezea hamu ya kujamiiana. Hivyo ili kuboresha afya yako ya kimapenzi jitahidi kutumia tunda hili.
 
Huzuia saratani

Utafiti umeonyesha kuwa virutubisho vinavyopatikana katika tunda la embe husaidia kuulinda mwili dhidi ya saratani mbalimbali kama vile saratani ya utumbo, matiti, tezi dume pamoja na saratani ya damu.
 
Huilinda ngozi

Embe linafaida kubwa katika afya ya ngozi. Kwani unaweza kupaka makapi yake usoni na kukaa nayo kwa muda usiopungua dakika 10 na baada ya hapo osha uso wako kwa maji yanayotiririka au yale yanayotoka bombani. Kwa kufanya hivyo kutakusaidia kuonekana na ngozi mbaya pamoja na kutibu tatizo la chunusi kama unalo pia.
 
Huboresha afya ya macho

Kikombe kimoja cha juisi ya embe kina 25% ya kiwango cha Vitamin A kinachohitajika mwilini kila siku. Hivyo kutumia juisi ya embe kutaboresha uwezo wako wa kuona nyakati zote, pamoja na kukuepusha na upofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…