Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam yakijaa maji kufuatia mvua mkubwa inayoendelea kunyesha tangu asubuhi, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kesho Mei 5, 2018 mvua hiyo itaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya jiji.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 4, 2018 na kubainisha kuwa maeneo mengine ambayo mvua hiyo itanyesha ni mikoa ya Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na kuambatana na upepo mkali.
 
Tahadhari zilizotolewa ni pamoja na mafuriko kutokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika sambamba na harati ya maisha kutokana na maji kujaa na kupita kwa kasi kushauri wanaokaa maeneo yanayojaa maji kuchukua tahadhari.
 
Upepo na mawimbi makali yatakuwapo katika maeneo ya ukanda wa Pwani inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,” imesema taarifa hiyo.

Mvua inayoendelea kunyesha leo imesababisha adha mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa usafiri katika baadhi ya maeneo kutokana na barabara kutopitika baada ya kujaa maji.
 
Watu wengi hupata kwikwi ingawa wapo wanapiga kwa muda mrefu zaidi kiasi cha kutia shaka.

Kwikwi husababishwa na kusinyaa kusiko kwa hiyari kwa kiwambo cha hewa kinachotenganisha kifua na sehemu ya tumbo. Kiwambo hicho kina umuhimu mkubwa sana katika upumuaji wa binadamu na kitaalamu huitwa diaphragm.
 
Wakati mwingine kwikwi huwa ni dalili ya ugonjwa fulani ambao haujabainika bado. Kwa watu wengi kwikwi huweza kutokea na kudumu kwa dakika chache tu na ni mara chache sana kwikwi hudumu kwa miezi na inapotokea inaweza kusababisha kuchoka na kupungua uzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…