Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

The new Kanye- mfuasi wa Trump anayeamini kuwa Waafrika waliopelekwa utumwani Marekani walichagua wenyewe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
View attachment 765902
meekmill-20180502-0001.jpg
 
Sababu hatarishi

Kwa ujumla wanaume hupatwa na kwikwi za muda mrefu mara nyingi zaidi ikilinganishwa na wanawake. Zipo sababu nyingi nyingine za kupata kwikwi ambazo kila mmoja anapaswa kuzifahamu ili kuchukua hatua pale inapolazimu.
 
Magonjwa ya akili ama hisia yanayotokana na uchovu wa akili au msongo wa mawazo pia vinahusishwa na kutokea kwa kwikwi ambazo zinaweza kuwa ama za muda mrefu au mfupi.

Baadhi ya watu wanaofanyiwa upasuaji hupatwa na kwikwi za muda mrefu baada ya kutumia dawa usingizi kabla ya upasuaji
 
Madhara

Kuendelea kwa kwikwi kwa muda mrefu kunaweza kuingiliana na ulaji wa chakula, ulalaji, uongeaji au uponaji wa kidonda baada ya upasuaji.

Ni vizuri kuidhibiti hali hii kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza na kuongeza uwezekano wa kutokea kwa madhara makubwa zaidi kwa mgonjwa.
 
Matibabu

Mara nyingi kwikwi huisha yenyewe bila kuhitaji matibabu, hata hivyo, kama kuna ugonjwa unaosababisha kwikwi hizo matibabu ya ugonjwa ni muhimu sana.

Yapo matibabu yanayoshauriwa kama kwikwi zimeendelea mfululizo kwa zaidi ya siku mbili. Mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutumia au kufanyiwa upasuaji mdogo.
 
Upasuaji huweza kufanyika ili kudhibiti mshipa wa fahamu unaohudumia kiwambo cha hewa na hutolewa baada ya dawa kushindwa kuitibu kwikwi husika.

Ingawa hakuna njia ya moja kwa moja ya kuisimamisha kwikwi, unapokuwa na kwikwi inayoendelea kwa kitambo unaweza kufanya kutafuta nafuu kwa kuzingatia kadhaa zinazopendekezwa na wataalamu.

Unashauriwa kuzuia pumzi kwa muda ukae bila kuhema au kunywa maji baridi.

Kama una kwikwi sugu, mabadiliko ya mtindo wa maisha inaweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo. Miongoni mwa unayotakiwa kuyafanya ni kuepuka vinywaji vya jamii ya soda na vyakula vyenye gesi. Vilevile, kula kiasi kidogo cha chakula.
 
Back
Top Bottom