Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwikwi yenyewe ni dalili inayojitegemea ambayo inaweza kuambatana na kubana kwa kifua, koo na tumbo.

Ni muhimu kumuona daktari kama unapata kwikwi inayodumu kwa saa 48 au inasababisha matatizo kwenye kula, kulala ama kupumua kiasi cha kukufanya ushindwe kfanya mambo mengine.
 
Sababu

Vitu ambavyo huweza kusababisha kwikwi inayodumu kwa muda usiozidi masaa 48 ni pamoja na unywaji wa vinywaji vyenye asili ya soda (carbonated beverages), pombe nyingi na ulaji wa chakula kingi.

Sababu nyingine ni mabadiliko ya joto, kumeza jojo pamoja na hewa.
 
Kwa upande mwingine, kwikwi ambazo hudumu kwa zaidi ya saa 48 huweza kusababishwa na vitu mbalimbali ambavyo kwa urahisi viko kwenye makundi kadhaa.

Miongoni mwa sababu hizo ni kuumia au kujeruhiwa kwa mshipa wa fahamu. Inapotokea kwa namna yoyote mishipa ya fahamu inayohudumia kiwambo cha hewa imeumia ama kujeruhiwa mtu huweza kupata kwikwi endelevu.
 
Miongoni mwa sababu zinazoweza kuumiza mishipa hiyo ya fahamu ni nywele ama kitu chochote kilichopo sikioni na kinachogusa ngoma ya sikio au uvimbe au goita shingoni. Lakini wapo wanaoweza kupata hali hiyo kutokana na kucheua au kuwa na maambukizi ya muda mrefu ya koo.
 
Nyingine ni magonjwa kwenye mfumo mkuu wa fahamu ambayo ni sababu nyingine ya kwikwi endelevu. Kunapokuwa na uvimbe au maambukizi kwenye mfumo mkuu wa fahamu wa mwili, huweza kusababisha kwikwi endelevu kwani magonjwa huharibu mfumo wa mwili wa kuidhibti kwikwi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…