Upasuaji huweza kufanyika ili kudhibiti mshipa wa fahamu unaohudumia kiwambo cha hewa na hutolewa baada ya dawa kushindwa kuitibu kwikwi husika.
Ingawa hakuna njia ya moja kwa moja ya kuisimamisha kwikwi, unapokuwa na kwikwi inayoendelea kwa kitambo unaweza kufanya kutafuta nafuu kwa kuzingatia kadhaa zinazopendekezwa na wataalamu.
Unashauriwa kuzuia pumzi kwa muda ukae bila kuhema au kunywa maji baridi.
Kama una kwikwi sugu, mabadiliko ya mtindo wa maisha inaweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo. Miongoni mwa unayotakiwa kuyafanya ni kuepuka vinywaji vya jamii ya soda na vyakula vyenye gesi. Vilevile, kula kiasi kidogo cha chakula.