Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.
 
Ni vizuri kuepuka kuvaa viatu virefu sana mara kwa mara na hasa kama unatembea navyo kwa muda mrefu maana husababisha matatizo kwenye misuli ya miguu kama vikivaliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia ni vyema kutovaa viatu vya kufunika na vyenye joto sana kwa muda mrefu hasa sehemu zenye joto kali maana huweza leta matatizo kwenye miguu. Vile vile si vyema kuvaa viatu vya wazi nje kama sehemu inabaridi kali na barafu.
 
Ili miguu yako iweze kuwa na uzuri wa asili siku zote basi ni vizuri angalau mara moja kwa wiki uwe na siku maalumu ya kusafisha miguu yako (sio kwamba siku nyingine husafishi, la hasha hapa naongelea usafi maalum). Andaa maji ya uvuguvugu na uweke nyenye beseni pamoja na sabuni ya maji ambayo ina dawa (medicated). Kisha kata kucha zako vizuri na kama utapendelea basi uisugue miguu yako kwa kutumia mafuta maalumu ya kusugulia kuanzia kwenye magoti hadi vidoleni (scrub).Kisha loweka kwenye maji kwa muda wa dakika tano.
 
Baada ya hapo nawa vizuri na kusugua unyayo kwa kifaa maalumu au jiwe laini kisha suuza miguu yako na maji safi. Baada ya hapo kausha vizuri na upake mafuta mazuri kwa ajili ya kulinda ngozi ya miguu. Hakikisha uchafu wote umetoka na hasa kwenye kucha na vidole.

Tunza miguu yako vizuri maana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
 
MGUU

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
 
Mwili wa binadamu hutawaliwa na mifumo ya neva au kwa kitaalamu Nervous System, ambapo katika mifumo hii kuna mfumo mkuu, central nervous system (ubongo na uti wa mgongo) na pia kuna mfumo wa pembezoni ambao ni kazi za mwili mbali na ubongo na uti wa mgongo (peripheral nervous system), mfumo huu wa pembezoni hujumuisha kazi za misuli, mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula tumboni, uwezo wa kuhisi baridi/joto, kugusa vitu na kujua ukali wa ncha ya kitu na kadhalika.
 
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
 
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo: Mtu kuhisi ganzi, maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi, kuhisi kama umevaa soksi au gloves wakati hujavaa, kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole, kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…