Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tunda la Kiwi (Chinese gooseberry/Yangtao) huzalishwa zaidi katika nchi ya New Zealand na lilianza kulimwa katika nchi hiyo miaka ya 1906. Tunda hilo liianza kuitwa 'Kiwi' na wamarekani katika miaka ya 1960s. Zipo aina 400 za tunda hilo nchini China ambako ndiko asili yake.
 
Tunda la kiwi lina enzyme iitwayo Actinidin ambayo kuvunja vunja proteins katika bidhaa zitokanazo na maziwa (dairy products) na huweza kutumika kulainisha nyama kwa kusugua nyama kwa kipande cha tunda hilo. Hivyo ni murua kwa wale wachoma nyama yaani nyamachoma.
 
Tunda la kiwi huweza kutumika kama tiba ya magonjwa au matatizo mbalimbali ya kiafya kama ifuatavyo:
Kuongeza kinga ya mwili dhidi ya virus na kutumika kama Health vitamin tonic. Kwa watu wenye kuhitaji kuongeza kinga ya mwili mathalani wenye maambukizi ya virus vya HIV watengeneze juisi hii: blend kwa pamoja matunda 2 ya kiwi, machungwa 1 - 2, limau nusu kipande, matunda 2 ya apple, matunda ya zabibu yapatayo 12, karoti moja ukubwa wa wastani na kisha miminia matone machache ya Echinacea tincture.
 
Kunywa kila siku.Pia watu wenye virus vya HIV wanapaswa kubadili aina ya vyakula wanavyokula. Waepuke kula vyakula kama nyama na mayai na kula vyakula vya mimea kama karoti, parachichi, cabbage, na saladi pamoja na fresh garlic na unga kidogo wa dried sea weed.
 
Balungi (Grapefruit) ni tunda ambalo lina wingi wa asidi ya citric, potassium na calcium. Unapokula tunda hili usiku wakati wa kwenda kulala hukufanya upande usingizi mnono. Unywaji wa juisi ya tunda hili asubuhi kabla ya kula chakula chochote hutibu tatizo la kutopata haja kubwa (constipation). kadhalika ulaji wa tunda hili hupunguza homa itokanayo na mafua makali (colds and flu). Uchachu uliomo kwenye tunda hili husaidia tumbo kuachilia kwa wingi vimen'genya vinavyosaga chakula (digestive enzymes).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…