Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na kwenye shina la kibofu cha mkojo na mwanzo wa mrija wa mkojo (urethra). Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume. Tezi dume ina upana wa takriban 3.8 cm, urefu 2.5cm na uzito takriban 25 grams.
 
Takriban theluthi moja (1/3) ya wanaume wote duniani waliovuka umri wa miaka 50 wana matatizo ya tezi dume. Hali hii huongezeka kufikia asilimia 75 kwa wanaume wenye umri wa miaka 80. Matatizo ya kuvimba kwa tezi na matatizo ya ufanyaji kazi wa kibofu cha mkojo (bladder disorders) huweza kusababisha magonjwa kama maumivu ya viungo vya mwili (arthritis), matatizo ya figo (kidney disorders) na uremia.
 
Tezi dume ni muhimu katika utoaji wa mkojo kwenye kibofu cha mkojo. Pia kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.
 
Kuvimba Tezi Dume (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH.
 
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
 
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…