Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maoni yako ni mazuri. Tutayafikiria na kuyafanyia kazi hivi karibuni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ijumaa Kenya inatarajiwa kuweka historia kwa kuwa na setilaiti ya kwanza kuwahi kutengenezwa nchini humo itayotumwa katika sayari.

Chombo hicho cha kuzunguka sayari kilitengenezwa na wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na shirika la teknolojia za sayari la Japan Space Agency (JAXA).
 
Naibu makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Mbithi amesema mafanikio hayo ni dhihirisho ya hatua zilizopigwa nchini kuhusu utafiti wa kiteknolojia ambao unaweza kuchangia katika maendeleo yatakayokuza uchumi wa kitaifa.
Setilaiti hiyo yenye ukubwa wa sentimita kumi kimchemraba itarushwa kwenye sayari kutoka kituo kilichopo Japan, lakini Wakenya kadhaa watapewa nafasi kushuhudia matukio hayo katika Chuo Kikuu cha Nairobi na yatarushwa moja kwa moja.
 
Kutakuwa na tukio Japan, katika sayari na hapa chuoni kile kitakachofanyika Japan kitashuhudiwa na baadhi ya Wakenya ambao watakuwa huko. Hapa tutakuwa na hafla katika ukumbi ambako matukio yatarushwa moja kwa moja. Tunasubiri siku hiyo kwa hamu,” amesema Profesa Mbithi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…