Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Stoke City Paul Lambert anatarajiwa kubaki katika kikosi hicho licha ya kupata matokeo mabaya msimu huu.

Mshambuliaji mrefu Peter Crouch na kipa wa Jack Butland waliongoza vilio kwa wachezaji wa timu hiyo baada ya mwamuzi Martin Atkinson kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo.
 
Baada ya filimbi hiyo, wachezaji wa Stoke City walilibujikwa machozi na wengine walishindwa kutoka uwanjani mapema kabla ya kupata usaidizi kutoka kwa wenzao.

Pia mashabiki wa klabu hiyo wakiwemo watoto walishindwa kujizuia kutokwa machozi kadri dakika za mchezo huo zilivyokuwa zikiyoyoma kabla ya filimbi ya mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…