Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya filimbi hiyo, wachezaji wa Stoke City walilibujikwa machozi na wengine walishindwa kutoka uwanjani mapema kabla ya kupata usaidizi kutoka kwa wenzao.

Pia mashabiki wa klabu hiyo wakiwemo watoto walishindwa kujizuia kutokwa machozi kadri dakika za mchezo huo zilivyokuwa zikiyoyoma kabla ya filimbi ya mwisho.
 
Stoke City ikicheza nyumbani, iliduwazwa kwa mabao yaliyofungwa na wachezaji James McArthur na Patrick van Aanholt.

Awali, Stoke City ilianza kupata bao lililofungwa na Xherdan Shaqiri, lakini timu hiyo ilishindwa kulinda ushindi wake katika mchezo huo.
 
Timu hiyo iliyoanzishwa miaka 155 iliyopita, haikuwa na matokeo mazuri msimu huu na imeporomoka ikiwa na pointi 30.

Ingawa Lambert atabaki Stoke City, lakini anatarajiwa kuwapoteza nyota sita wa kikosi cha kwanza ambao hawatakubali kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
 
Timu hiyo iliyoanzishwa miaka 155 iliyopita, haikuwa na matokeo mazuri msimu huu na imeporomoka ikiwa na pointi 30.

Ingawa Lambert atabaki Stoke City, lakini anatarajiwa kuwapoteza nyota sita wa kikosi cha kwanza ambao hawatakubali kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
 
Baadhi ya nyota wanaotarajiwa kuondoka ni Joe Allen, Xherdan Shaqiri, Badou Ndiaye na Jack Butland .

Charlie Adam, Glen Johnson, Stephen Ireland na Ibrahim Afellay wanaweza kuondoka kwa kuwa walicheza kwa mkopo.
 
Beki Kurt Zouma anatarajiwa kurejea Chelsea baada ya kutolewa kwa mkopo na kocha Mtaliano Antonio Conte.

“Ukirejea matokeo ya mwezi Julai na Agosti, hatukuwa kwenye kiwango bora, unaposhindwa kupata ushindi katika kipindi hicho lazima utakuwa kwenye matatizo,” alisema Lambert
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…