Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtahiniwa Kidato cha Sita Ajinyonga

Mwakasege Blog / 2 days ago



Siku moja kabla ya kuanza mitihani ya kidato cha sita, mtahiniwa wa Shule ya Sekondari Nyakato, Robert Masaba (21) amekufa ikidaiwa kuwa amejinyonga.


Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018 hadi Mei 25, 2018.


Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai Masaba amejinyonga usiku wa kuamkia leo Mei 6, 2018 kwenye mwembe akiwa Shule ya Sekondari Kahororo.


Masaba na wenzake walihamishiwa shuleni Kahororo zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya sekondari ya Nyakato kuathiriwa na tetemeko la ardhi.


Mkuu wa Shule ya Kahororo, Omary Rugambaki amezungumzia tukio hilo akisema polisi wameshafika kwa uchunguzi.


Visit website
 
Zari azidi kuumizwa na kifo cha aliyekuwa mume wake, Ivan

Mwakasege Blog / 2 days ago



Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady ameonyesha ni kiasi gani anamkumbuka aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ ambaye ni Marehemu kwa sasa.


Zari ameshare picha ya zamani katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha Don akiwa na mwanaye, Pinto ambaye ni mkubwa kwa sasa na kuandika;


"Ni vigumu kuamia ni takribani mwaka mmoja sasa tangu Mungu alipokuita, naona ni kama jana. Hakuna siku inayopita bila kukuombea pamoja na mama yako. Roho zenu ziendelee kupumzika kwa amani.Hakika sisi huja kutoka mbali. Hapa Don anaonekana amembeba Pinto (ambaye ni mkubwa sasa), alianza naye kutoka mbali."


"Can’t believe its almost a year since God called you, it seems like yesterday. No day passes that i don’t pray for you and mom. May your souls continue resting in peace.

We surely come from far. Here Don is seen carrying Pinto ( who is a giant now), started from the botton right? Your missed[emoji257][HASHTAG]#RandomPost[/HASHTAG]"


Ivan alifariki May 25, 2017, alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

Visit website
 
Kambi ya Upinzani waitaka Serikali kuwasikiliza marais wastaafu JK na Mkapa

Mwakasege Blog / 3 days ago



Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wameitaka Serikali kutilia mkazo ushauri uliotolewa na marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wa kuwapo kwa mjadala wa kitaifa wa elimu.


Wakizungumza leo Mei 5, 2018 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, wabunge wa upinzani wamesema hali ya elimu ni mbaya na Serikali inaandaa kizazi kijacho kisichoweza kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.


Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema, “Taifa lolote lile ambalo halijui umuhimu au halipendi kuwekeza katika elimu ni Taifa mfu, ukitaka kuua elimu yetu basi usiwekeze katika elimu.”


Mbatia ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa amesema, Taifa hili limebahatika kuwa na marais walimu isipokuwa Mzee Mkapa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ni Mwalimu, ‘First Lady’ Janeth Magufuli ni mwalimu.


“Leo Tanzania tupo wapi? Na rasilimali kubwa kuliko zote duniani ni rasilimali watu na rasilimali watu tuliyonayo sasa haijitambui na ili ilijitambue lazima iwe na ufahamu.


“Kama Rais Mkapa anaomba mjadala wa elimu na amekuwa akilirudia mara kwa mara. Rais Kikwete amezungumza haya. Rais Mwinyi amesema nchi inaongozwa kama gari bovu. Mwalimu Nyerere alilisema hadi anaingia kaburini,” amesema Mbatia na kuongeza:


“Tuwe na mjadala mpana wa kitaifa, Tanzania ni yetu sote, watoto hawa wanaumia, hivi ukweli watoto wa rais wetu wanasoma katika shule hizi hizi, hebu tumwogope Mwenyezi Mungu.”


Mbatia amesema vitabu vinavyosambazwa sasa shule za msingi ni vibovu na kumtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako kuacha kutoa vitisho kwa watu kuwa watachukuliwa hatua na badala yake, “ajiulize tatizo lipo wapi, nani kalisababisha.”


Naye Waziri kivuli wa elimu, sayansi na teknolojia, Susan Lyimo amesema; “Hakuna nchi yoyote iliyoendelea pasina kuwekeza katika elimu, lakini kinachofanyika sasa, ingawa Serikali haitaki kusikia ila hali ya elimu ni mbaya.”

Visit website
 
Shidaaaaaaaaa
 
Mwigulu Nchemba: Wasioridhishwa na utendaji wa polisi waripoti kwangu

Mwakasege Blog / 4 days ago



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wasioridhishwa na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kukata rufaa kwake.


Pia, amewataka wanasiasa wanaozungumzia matukio ya kupotea watu kuwa na ushahidi wa kutosha na kama hawana wasiyazungumze kwani yanajenga taswira hasi kwa nchi.


Ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 na kubainisha kuwa si askari wote ni wema na kwamba wanaokiuka taratibu za kazi hatua zitachukuliwa dhidi yao.


“Damu ya mwanadamu haiwezi kulinganishwa na thamani ya chama chochote au kabila lolote na sisi hatutakubali damu imwagike bure lakini panapotokea tatizo la kiutendaji la aina hiyo, hilo ni la mtu mmoja,” amesema.


Kuhusu watu wanaopotea amesema, “Kuna mambo mengi ya kimaadili tumeyafanyia msako, kuna watu wamehama majumbani mwao kwa msako wa dawa za kulevya na wengine tumeambiwa wamevuka mipaka ya nchi yao na ndio hao wanasema wamepotea na ukituuliza yuko wapi na sisi tutasema yupo wapi.”


Amesema kuna ambao wamekimbia baada ya baadhi ya watu waliokamatwa kuwataja kuwa wanatumia silaha.


“Ukijumlisha hao ambao hawapo na kusema wamekufa hiyo siyo sawa kwani kwa sasa Watanzania ambao wanashikiliwa nje ya nchi katika magereza ni zaidi ya 1,000. Ukisema hao watu wameuawa ni makosa,” amesema.

Visit website
 
Tamko Rasmi la Wizara Ya Elimu Kuhusu Kitabu Kinachosambazwa Mitandaoni

Mwakasege Blog / 4 days ago



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeibuka na kukanusha vikali kuwa kitabu kinachosambazwa katika mitandao ya kijamii kinachoelezea viungo vya mwanadamu sio chapisho la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wala sio miongoni mwa vitabu ambavyo vimesambazwa shuleni.


Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Elimu Mwasu Sware hii leo Mei 04, 2018 baada ya kusambazwa picha hiyo katika mitandao ya kijamii na kupelekea kuzua mjadala mzito kwa wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu nchini jambo ambalo wamedai ndiyo sababu pekee ya elimu ya Tanzani kudidimia.


"Kitabu hicho hakina uhusiano wowote wala hakifanani na vitabu ambavyo vimechapishwa hivi karibuni na TET. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawasihi watanzania kupuuza taarifa hizo ambazo siyo za kweli na zina nia ya kupotosha na kuleta usumbufu kwa jamii", amesema Sware.


Soma hapa chini habari kamili kuhusiana na taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia



Visit website
 
Ramadhani Malima Naye Asimamishwa Kuchezea Mbeya City

Mwakasege Blog / 4 days ago



Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, imetangaza kumsimamisha beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima, kwa kosa la kurudi Uwanjani kushangilia wakati akiwa amepewa kadi nyekundu.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 22 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Bodi imetangaza kumsimamisha mchezaji huyo kuichezea Mbeya City mpaka pale shauri lake litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF kisha kutolewa maamuzi.

Mchezaji huyo alipewa kadi ya pili ya njano na nyekundu kufuatia kucheza madhambi dhidi ya mchezaji wa Yanga zikiwa zimesalia dakika chache mpira kumalizika.

Mchezo huo uliofanyika Mbeya, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Visit website
 
Msigwa Aeleza Sababu za Kummwagia SIFA Rais Magufuli

Mwakasege Blog / 4 days ago



Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amemsifu Rais John Magufuli kwa kupeleka fedha za maendeleo katika halmashauri yake bila ya kubagua, lakini amesema video iliyosambaa mitandaoni haitoi picha halisi ya alichosema.


Video hiyo fupi inamuonyesha Mchungaji Msigwa akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika Ikulu ya Iringa juzi na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, wa kisiasa na kidini.


“Na Mheshimiwa Rais umekuwa ukisisitiza kwenye hotuba zako kwamba wewe hujali vyama na hili limedhihirika kwa kweli kwamba hujali vyama,” anasema Mchungaji Msigwa katika video hiyo huku waalikwa wakimpigia makofi.


“Umesaidia sana. Bahati mbaya hawakukupangia ratiba ya kufungua miradi. Hela za kutoka kwako zimekuja nyingi. Amezungumza Mheshimiwa (Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine) Mahiga, tuna barabara nzuri.


“Katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais tumejenga barabara ya lami ya mradi wa World Bank kutoka Mlandege mpaka kwa mkuu wa wilaya, karibu Sh3.5 bilioni, tuna stendi nzuri iko hapo chini Ipogolo, karibu Sh3 bilioni. Tuna maji. Kwa hiyo kuna vitu vimefanyika.


“Kwa kweli Mheshimiwa Rais hupendelei, hata sisi wa Chadema unaleta hela. Kwa hiyo wewe hujali vyama. Unaleta hela. Kwa hiyo wewe huwa hujali vyama hilo nikupongeze sana.”


Wakati akisema hayo, picha zinaonyesha waalikwa wakiangua vicheko na sauti zao zinasikika wakati akihitimisha hotuba yake.


Msigwa ni mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali ya Awamu ya Tano na alipotafutwa kuelezea kwa kirefu alichokizungumza alisema, “Wamechukua kipande kidogo ambacho nilisema hela zimeletwa Manispaa ya Iringa, lakini wameacha kipande kikubwa ambacho nilizungumza kwamba hata kama madiwani wameondoka, Manispaa ya Iringa imekuwa nzuri, imekuwa bora,” alisema jana.


“(Wanachama wa Chadema na Ukawa) Wasione kama kuna mtu hapa ameyumba au nimesalimu amri. Mapambano bado yanaendelea, hiyo ndiyo hoja.”


Kuhusu alichokizungumza, alisema kauli yake ilimaanisha kuwa Manispaa ya Iringa imekuwa bora katika kipindi hiki ambacho imekuwa chini ya Chadema kwa kuwa Rais amekuwa akipeleka fedha bila ya kujali vyama, lakini akashangaa kwamba ratiba yake mkoani Iringa haikujumuisha kutembelea miradi mikubwa kama barabara, machinjio kubwa kuliko zote Tanzania, stendi na mambo mengine.


“Kuna miradi mingi imefanyika chini ya uongozi wetu ambayo haihusiani na uwepo wa CCM ambao wapo katika manispaa hii na kumekuwa na dhana kuwa watu wakiwa Chadema au kiongozi akiwa Chadema, hakuna maendeleo na ndio maana madiwani wamekuwa wakihama,” alisema.


“Kwa mfano, tuna barabara ambayo imejengwa kwa Sh3.5 bilioni na ambayo haikuwapo. Tumejenga katika kipindi hiki ambacho manispaa inaongozwa na Chadema.”


Pia alisema kuna machinjio ambayo itakuwa kubwa kuliko zote katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pamoja na stendi ya mabasi iliyokamilika.

Visit website
 
Manara apewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu, aomba radhi

Mwakasege Blog / 4 days ago



Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amepewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.


Manara amepewa barua iliyomuonya kutokana na kukiuka sheria za michezo za ligi kuu mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.


Mtendaji Mkuu wa Bodi Ligi, Boniface Wambura ameeleza kuwa uamuzi huo umeafikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichopitia taarifa na matukio mbalimbali ya ligi msimu wa 2017/18 yanayoendelea kulindima hivi sasa, ambapo kilibaini tukio la utovu wa kinidhamu kwa afisa huyo.


“Katika mechi namba 178 dhidi ya Yanga SC iliyochezwa Aprili 29, 2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa aliingia uwanjani Haji Manara kushangilia ushindi wa timu yake. Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo, inayozuia wasiohusika kuingia uwanjani kabla, baada na wakati mechi ikiendelea”, amesema Wambura.


Kwa upande wake, Haji Manara ameonesha kulitambua kosa lake na kuiomba radhi Bodi ya Ligi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), pamoja na wadau wote wa soka, huku akieleza kuwa furaha ndiyo iliyompelekea yeye kutenda kosa hilo.


“Muungwana akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa mshabiki kama kumgalagaza mtani…it will never happen again..ila sijui itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwali[emoji16][emoji16][emoji16] @tanfootball [HASHTAG]#bodiyaligi[/HASHTAG] [emoji120][emoji120]” ameandika Haji Manara karika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.


Katika Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa namashabiki wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini, Simba iliibuka kidedea baada ya kuichapa Yanga goli 1 ambalo lilifungwa dakika ya 37 na Erasto Nyoni.



Visit website
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…