Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JIWE kuu limeng’oka. Kocha mkongwe wa Arsenal, Arsene Wenger ameaga rasmi tena kibabe kwenye Uwanja wa Emirates juzi, na sasa amebakisha dakika 90 tu za kuwa kocha wa Arsenal akisubiri pambano la mwisho dhidi ya Huddersfield ugenini.
 
Historia yake ya Emirates imemalizika juzi jioni katika pambano la Burnley na msimu ujao kiti chake kitakaliwa na mtu mwingine lakini sio yeye. Miaka yake 22 Emirates imefikia kikomo juzi jioni na Arsenal walimuaga vizuri ndani na nje ya uwanja.
 
Wakati ndani ya uwanja Arsenal walishinda 5-0, nje ya uwanja mashabiki waliujaza uwanja na kuvaa fulana za kumuaga zilizoandikwa ‘Merci Arsene’ huku wakiimba wimbo wao maarufu wa “Kuna Arsene Wenger mmoja tu”.
 
Mara baada ya pambano hilo, Wenger alizungumza na mashabiki waliojitokeza uwanjani akitoa hotuba yenye hisia kali kwa ajili ya kuwaaga mashabiki hao ambao wamekuwa sehemu ya maisha yake kwa muda mrefu tangu alipowasili klabuni hapo mwaka 1996.
 
Asanteni sana. kabla sijaanza, nataka kumtakia kila la kheri kocha mwenzangu, Sir Alex Ferguson. Asante kwa kuwa na mimi kwa muda mrefu. Najua sio rahisi. Juu ya yote, mimi kama ninyi, ni mshabiki wa Arsenal,” alisema Wenger.
 
Hili ni zaidi ya suala la kutazama mpira tu, ni njia ya maisha.

“Ni suala la kujali mchezo huu unaovutia, dhidi ya imani tulizojiwekea. Soka ni kitu ambacho kinaingia katika miili yetu, katika kila chembechembe za damu.
 
Tuna wasiwasi, tunajali, tunatamani, lakini unapokuja hapa, kituo cha ndoto zetu, tunafahamu soka ina maana gani.”

“”Ningependa kumshukuru kila mtu klabuni, nitawakaribisha, nitawasukuma hawa wachezaji na wafanyakazi ambao walikuwa nyuma yangu, hili kundi la wachezaji hapa lina ubora sana. sio tu uwanjani bali hata nje ya uwanja. Tafadhali ipeni sapoti hii timu kwa sababu inastahili.
 
Mourinho na mabosi wa Man United wameanza kupambana kusaka dawa ya kumzima Guardiola, ambapo harakati za kuingia na kutoka sambamba na vikao zimeshika kasi pale Old Trafford. Msimu huu Mourinho amekuwa mnyonge mbele ya Guardiola ambaye kikosi chake kimeuwasha moto kwelikweli na kutangaza ubingwa mapema kwa tofauti ya pointi 13 huku akiwa amepoteza michezo miwili tu.
 
Katika michezo hiyo aliyopoteza Guardiola mmoja amechapwa na Liverpool kwa mabao 4-3 kisha akachapwa na Man United mabao 3-2, ambapo kama Man United ingepoteza mchezo huo basi City ingetangaza ubingwa wake mbele ya United tena ndani ya Old Trafford.
 
Lakini, ishu kubwa inayoendelea Old Trafford kwa sasa ni usajili wa mastaa wa nguvu barani Ulaya, ambapo Mourinho na Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Ed Woodward wamejifungia na kutengeneza orodha moja matata ya mastaa ambao watakwenda kuvaa jezi za United msimu ujao.
 
Jose anataka kujenga kikosi matata kitakachotoa ushindani mbele ya vigogo wengine barani Ulaya kama Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, PSG na Manchester City ambayo imekuwa ikiwasumbua tangu ilipoanza kunolewa na Guardiola.
 
Orodha ya mastaa hao kama Mourinho atafanikiwa kuwanasa wote basi ni tishio kubwa kama tetemeko na kamwe usiombe ukakutana nayo uwanjani ni lazima bao za kutosha zitakuhusu.
 
Back
Top Bottom