myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
07:38
Ikiwa wahusika wapo wanajizubaisha, si kosa kutumia fursa. Sisi hatuoni umuhimu wa kujitangaza kimataifa acha wengine wajitangaze kwa niaba yetu huenda tukajifunzaWakenya wanachekesha sana wanasema Kiswahili ni chao, Na wao ndiyo wamefanya Lugha ya Kiswahili itambulike na ianze kutumiwa rasmi ktk Twitter. Mmiliki wa Twitter Jack Dorsey amekitambua Kiswahili kwamba kinazungumzwa na watu zaidi ya mil 200, na Ktk Twitter, Kiswahili kinatumiwa na watu milioni 50. Wakenya wanasema watu mil 50 ni wao wanaozungumza kiswahili ktk Twitter.
Ligi ya mpira wa miguu Hispania (LA LIGA) nayo imetupia post nne juzi ktk Twitter kwa Kiswahili.
WAKENYA: Mara waseme Ali Kiba na Diamond ni Wakenya, Mara mlima Kilimanjaro ni wao, Du! Jamaa hawaishiwi na vituko.