Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii ndio Sababu wagonjwa kuacha kutumia ARVs

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago

LUGHA chafu, unyanyapaa na kutoa siri za wagonjwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa vituo vya afya, vimetajwa kuchangia wananchi kutojitokeza kupima afya, huku wagonjwa wa Ukimwi wakiacha kutumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs).

Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA), Justine Mwinuka, wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wanne wa VVU na Ukimwi katika sekta ya afya na sherehe za miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi.

Mwinuka alisema vitendo vya kutoa siri za wagonjwa, lugha chafu na unyanyapaa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa afya ni miongoni mwa mambo yanayochangia watu wengi kushindwa kufika kwenye vituo hivyo kupima afya zao na wengine kuacha kutumia dawa.

“Mheshimiwa Waziri, changamoto hizi na nyingine huzorotesha upatikanaji wa matokeo yaliyotarajiwa ya matibabu ya kufubaza virusi, kwa kuwa huchangia watu kutokwenda vituoni kabisa au kuacha matibabu,” alisema Mwinuka.

Alisema lugha za kejeli za kuwabeza wagonjwa wanaofika kupata huduma, dawa za kufubaza virusi zimechangia kwa wagonjwa kutoendelea kufika vituo hivyo kupata matibabu hasa kundi la vijana.

Mwinuka alitaja changamoto zingine ni upatikanaji wa dawa za magonjwa nyemelezi na kuiomba serikali kusaidia upatikanaji wa dawa hizo, kuboreshwa zaidi pamoja na kutumia muda mwingi kwenye vituo hivyo kusubiri matibabu.

Changamoto zingine ni umbali wa vituo vya kutolea ARVs hasa maeneo ya vijijini, wagonjwa kuachwa vituoni bila kupewa huduma na kuzuiliwa kuchukulia dawa.

Akizindua mpango huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema hajaridhishwa na takwimu za kupungua kwa maambukizi hayo nchini.

Mwalimu alisema kwa muda wa miaka mitano takwimu zinaonyesha maambukizi hayo yamepungua kwa asilimia 0.4 kutoka asilimia 5.1 hadi 4.7, kiasi ambacho ni kidogo sana.

Aidha, alisema wakati takwimu zikionyesha kuwa maambukizi ya kitaifa yanapungua, lakini takwimu za baadhi ya mikoa zinaonyesha kupanda zaidi kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Alitaja sababu zilizosababisha maambukizi kuongezeka ni kupungua kwa nguvu ya kampeni ya maambukizi katika mikoa iliyokuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa Ukimwi.

Naye, Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kupambana na Ukimwi, Dk. Angela Ramadhani, alisema malengo ya mkakati wa nne wa mapambano dhidi ya Ukimwi yanalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwahamasha walioambukizwa kutumia ARVs, ili kuzuia maambukizi zaidi.
 
Kuelekea kwa babu...
FB_IMG_1525825322808.jpg
 
VIDEO: Neema kuzidi kuongezeka, Mfumuko wa Bei Umeshuka kwa kasi

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago

Ofisi ya Takwimu imetoa taarifa kuhusiana na kushuka kwa mfumuko wa bei kwa mwezi April, 2018, ambapo kasi ya mfumuko wa bei imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioisha mwezi march.

Kupungua huko kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei ya bidhaa za vyakula ambavyo ni pamoja na mahindi kwa 5.2%, unga wa mahindi 5.6% mtama 7.3% unga wa mihogo 9.3%, maharage 9.2% na mihogo mibichi 13.2%

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE.......

CAF yairuhusu Yanga

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago

Shirikisho la soka Barani Africa CAF limeipa ruhusa klabu ya Yanga kutumian jezi zake zenye nembo ya wadhamini baada ya kuwawekea zuio kwenye mchezo dhidi ya U.S.M Alger wikiendi iliyopita.

Taarifa ya Klabu ya Yanga iliyotolewa jioni hii imeeleza kuwa, baada ya wao kuliandikia barua shirikisho hilo limewajibu kuwa wapo huru kutumia jezi zao hizo ambazo wamekuwa wakizitumia msimu huu wote.

''Rasmi, CAF wameiruhusu Yanga kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu wa timu Sportspesa kwenye mechi zake za hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Africa'', imeeleza taarifa hiyo.

Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza wa makundi jumapili iliyopita na kukubali kichapo cha mabao 4-0 ugenini. Katika mchezo huo Yanga walilazimika kutumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini.

Mchezo unaofuata wa Yanga kwenye hatua ya makundi utachezwa Mei 16 jijini Dar es salaam wakiwaalika Rayon Sport ya Rwanda na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
 
VIDEO: "Nakuacha kwasababu ni Mkurugenzi Mpya, nakupa siku 45 tu" Waziri Jafo

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapa siku 45 Meneja masoko na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kukamilisha changamoto zote za soko la Ferry jijini Dar es salaam.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Waziri Jafo atoa siku 45 kukamisha kukarabati soko la Ferry

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago

Waziri wa nchi ofisi ya Rais serikali za mitaa Tamisemi Mhe. Suleiman Jafo amtoa siku 45, kwa mamlaka husika katika soko la Ferry lililopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kufanya Ukarabati wa miundo mbinu ya soko hilo ambayo imeharibika na kusababisha mazingira magumu ya kazi kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo katika ziara aliyoifanya katika soko hilo ambapo amekagua miundo mbinu mbalimbali ikiwepo barabara, ya soko hilo,meza choo pamoja na maji ambapo amesema wafanyabiashara hao wanalipa kodi hivyo ni haki yao kuwepo kwa miundo mbinu rafiki na salama kwao.

"Nitakuja hapa baada ya siku 45, kuona mazingira yamerwkebishwa na nitoe maelekezo kwa Injinia ahakikishe barabara hii imetengenezwa na tarehe 23, mwezi Julai nitakuja hapa kuangalia utekelezaji ukarabati wa mazingira haya kwani hili ni soko kubwa ambalo linakuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla"Amesema Jafo.

Aidha amesema anataka wakina Mamantilie waliokuwa wakifanya biashara katika eneo hilo na kutolewa warudishwe na kuwataka akina Mamantilie hao kufuata sheria na kuwa mlinzi kwa kila mmoja kuhakikisha wanaofanya biashara za madawa ya kulevya wanabainishwa.

" Nataka wakina mama waliokuwa wanafanyabiashara ya chakula hapa Sokoni warudishwe na kuendelea na kazi zao ili kuwarahisishia wafanyabiashara kupata chakula kwa urahisi na kuwataka Mamantilie hao kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake ili kubaini wanaopita na kutumia madawa ya kulevya"Amesema

Waziri Jafo amesema kuwa ameuzunishwa na uongozi unavyofanya kazi katika eneo hilo kwani wananchi wanapata shida kutokana na miundo mbinu mibovu.

Pia amemtaka Meneja wa soko kuhakikisha wanatenga sehemu za wakina Mama Ntilie ili waendelee kufanya biashara kutokana na kutolewa maeneo hayo kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya Kulevya.

"Meneja wa Soko hakikisha mnatenga sehemu maalumu ya kina Mamantilie ili waweze kuendeleza biashara yao na wanaofanya shughuli zao hapa waweze kuwa na uhakika wa kupata chakula sehemu salaam na rahisi kwao"Amesema Waziri Jafo.

Pia ameutaka uongozi kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo katika soko hilo kwani ni sehemu kubwa ambayo wananchi wanaofanya biashara zao na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao,pamoja na kuinua uchumi wa nchi na si kusubiri waziri afike kutoa maelekezo.

Kwa Upande wake Meneja wa Soko la Ferry Mkuu .B. Hanje amesema kuna Jengo ambalo lipo katika soko hilo na kwamba linadaiwa kuwa ni la halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo hawakusanyi Kodi kutoka katika jengo hilo hivyo wanashindwa kulikarabati kutokana na kuwa liko chini ya manispaa.

Amesema watahakikisha yote aliyoyasema Mhe. Waziri yanafanyiwa kazi kikamilifu na kuondoa kero na changamoto zilizopo.

Nao wafanyabiashara wa soko hilo wamekiri kuwepo kwa changamoto hizo ,na wamemshukuru Mhe. Waziri kwa kufika na kuwasaidia ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa na kuweza kufanya kazi Katika mazingira rafiki na salaama ili kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom