Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1524313862900.jpg
 
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa, Sepp Blatter ni kama anaipigia ndogondogo Morocco kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2026 akisema haiwezekani Kombe la Dunia likaandaliwa na nchi zaidi ya moja.
 
Rais huyo wa zamani wa Fifa alisema alienguliwa kutokana na kile kilichoelezwa kashfa ya rushwa, amekuwa mstari wa mbele kuipigania Afrika kuandaa Fainali za Kombe la Dunia. Blatter wakati wa utawala wake, aliipigania Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mara ya kwanza 2010 na sasa anaonekana kuanza kampeni za 2026.
 
Hiyo pia ni kutokana na balozi wa Morocco kuzinadi fainali hizo kuwa ni El Hadj Diouf ambaye ana uhusiano na Samoura. Hata hivyo, Samoura alikanusha madai hayo. Kwa Blatter, 82, iko hivi. Fifa inataka kuandaa Fainali za Kombe la Dunia kwa kuanza na nchi 48 sasa ni wakati wa kutoa nafasi kwa nchi moja kuandaa na kuandaa kwa nchi mbili ni uamuzi mwingine. Hata hivyo, uamuzi wa kuandaa nchi moja ama mbili utatolewa Juni 13, mwaka huu.
 
Marekani, Canada na Mexico zimeungana pamoja kupambana na Morocco inayotaka kuwa mwenyeji na imesimama yenyewe.

“Kuwa na nchi kubwa tatu kwa pamoja. Ni wazi kwamba mmoja anaweza kuwa mwenyeji, sasa kwanini ziwe nchi tatu?” Blatter aliiambia Mani Djazmi, katika kipindi cha BBC’s World Football.
 
Blatter ambaye hakubaliani na uamuzi huo, aliiongoza Fifa kwa miaka 17 kabla ya kuenguliwa mwaka 2015.

Kombe la Dunia limewahi kuandaliwa na nchi mbili kama ilivyokuwa kwa Korea Kusini na Japan mwaka 2002, mashindano ambayo Blatter anasema yameichafua Fifa
 
Alisema uandaaji wa pamoja uliwahi kuombwa na Libya na Tunisia Fainali za 2010 na ukakataliwa, Hispania na Ureno na Ubelgiji na Uholanzi zilitaka fainali za 2018, na Fifa inataka nchi isimame peke yake.
 
Sasa iko hivi. Wenger katika taarifa yake alisema hataki tena kukaa kwenye benchi na kuanza kupiga kelele uwanjani kuwaongoza wachezaji. Hilo suala hataki na anataka kuanza maisha mengine kabisa badala ya uwanjani.
 
Pengine ninaweza kufikiria vinginevyo. ‘Hapana, Inaweza kuwa hivyo, au nikabadili mwelekeo ikawa vinginevyo’,” alisema Wenger. “Hicho ndicho ninachoiweza kusema kwa sasa. Huu ni wakati mwingine kwangu na nina kila sababu ya kuuweka hivyo.
 
Back
Top Bottom