Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.
 
REMBO HALISI WA MWANAMKE UNAANZIA NDANI YAKO

Urembo unajumuisha mambo mengi kwa mwanamke tofauti na dhana za watu wengi wanaofikiri kwamba urembo ni kuvaa vizuri, kuonekana vizuri na hata manukato mazuri, kuwa na umbo zuri, na jinsi unavyoonekana kutokana na umbo lako. La hasha hivi ni vidokezo vya urembo kwa mwanamke.
 
Urembo halisi ni amani na utulivu uliopo ndani yako, hali hii ina faida katika moyo wako na mwili wako pia. Jambo la msingi hapa ni kuwa na amani kwa kuepukana na msongo wa mawazo na kuwa mwenye furaha muda wote. Hali ya msongo wa mawazo (stress) huleta maradhi mbalimbali kama vidonda vya tumbo (gastric ulcers), shinikizo la damu (blood pressure) na mengine mengi
 
Katika maisha ya mwanamke yeyote mwenye kupenda urembo na muonekano mzuri ni pamoja na kuepukana na magonjwa yanayoepukika kwa njia ya kua na amani na furaha muda wote kwa kujenga sura nzuri, umbo zuri lenye kupendeza pale unapovaa nguo ya aina yoyote au kupaka vipodozi vya aina yoyote ile.
 
Ni vyema tujiulize, je ni kiasi gani cha fedha tunatumia kila mwaka kununua nguo mpya, viatu vya gharama, vipodozi na mikoba? Bila shaka ni gharama kubwa lakini je, kuna gharama gani tunatumia kujenga furaha na amani ndani yetu? Jibu ni rahisi tu furaha na amani ni wewe mwenyewe pasipo gharama yoyote ile. Maswali haya yatakufanya wewe kama mwanamke mpenda urembo kupata njia thabiti za kuongeza urembo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…