*Bread pudding* Bread pudding : katakata vipande ndogondogo mkate aina yeyote kama scones vipande tano, au slice za mkate kama 12, tia kwenye mkebe ya kuokea tia zabibu kavu kiasi unapenda. Changanya vizuri. Weka kando. kwenye bakuli kubwa piga nusu lita ya maziwa, mayai 4 kubwa, 3/4 C sukari au unavyopenda, vanilla kijiko moja ya kula, vijiko tatu ya kula siagi iliyoyayushwa. Piga mpaka zichanganyike vizuri, mimina kwenye mkate, changanya pamoja vizuri, nyunyuzia sukari juu ukipenda. oka mpaka iive, dakika 35-40 moto ya kati. SAUCE YA CUSTARD: Changanya vikombe tatu ya maziwa pamoja na vijiko 2 1/2 ya kula ya custard poda, sukari unavyopenda, kijiko moja ya chai iliki. Koroga pamoja kwa moto ya kati, mpaka ianze kuwa nzito. Epua kisha serve na pudding ikiwa moto.