Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
Screenshot_20180513-161436.jpg
 
Hoteli ya Nairobi itatoza kiingilio cha Sh1milioni kwa ajili ya kuona harusi ya Mwanamfalme Harry na Meghan Markle watakapofunga ndoa Jumamosi wiki hii ambayo itaonyeshwa moja kwa moja kwenye luninga.

Kiingilio hicho hakitalipwa kuingilia kwenye Ukumbi wa Windsor Castle nchini Uingereza bali ni pale itakapoonyeshwa moja kwa moja kupitia luninga za Kenya
 
Baada ya kutoa kiingilio hicho wateja watakaokata tiketi watapata fursa ya kulala kwenye hoteli ya Nairobi na pia watatembezwa kwa kutumia usafiri wa helikopta mpaka Mlima Kenya kwa ajili ya kupata kifungua kinywa na pia watapata chakula wakiwa hotelini.

Kwa mujibu wa matangazo hayo kila mteja ambaye atakuwa bibi na bwana watalala kwa siku mbili kwenye hoteli hiyo na asubuhi watachukuliwa kwa helikopta kuelekea Mlima Kenya kupata kifungua kinywa.
 
Taarifa hiyo ilisema kwamba nafasi zilizopo ni kwa bibi na bwana 20 pekee .

Harusi hiyo imekuwa kivutio kwa dunia nzima tangu kipindi cha kuvishana pete mpaka kufikia hatua ya kuoana kwa wapendwa hao.

Wawili hao walithibitisha rasmi uchumba wao Novemba na wakasema harusi yao itafanyika katika kanisa dogo la St George, Windsor Castle.
 
Tarehe ya harusi yao inaenda kinyume na utamaduni wa harusi za familia ya kifalme Uingereza ambazo hufanyika katikati ya wiki.

Familia ya kifalme nchini Uingereza itagharimia harusi hiyo, ikiwa ni pamoja na ibada yenyewe, muziki, maua na sherehe ya baada ya ibada.

Markle, ambaye ni mprotestanti, atabatizwa na kupewa kipaimara kabla ya harusi hiyo kufanyika.
 
Mwigizaji huyo Mmarekani pia anakusudia kuchukua uraia wa Uingereza.

Ofisa wa mawasiliano wa Mwanamfalme Harry Jason Knauf amesema kwamba Windsor ni "pahala maalum sana" kwa wawili hao, akisema walikaa huko kwa muda tangu walipokutana mara ya kwanza Julai 2016.
 
Sayari Ya Miller Iliyoigizwa Katika Baadhi Ya Filamu Ni Kweli Ipo. Sehemu Kubwa Ya Sayari Hiyo Imetawaliwa Na Kina Kifupi Cha Maji.
Ukikaa Huko Kwa Saa Moja Ni Sawa Na Miaka 7 Duniani.
Hivyo Kama Uliondoka Ukiwa Na Miaka 15 Pamoja Na Wenzako Uliowaacha Duniani, Na Ukakaa Huko Kwa Saa 10.
Ukirudi Duniani Utakuwa Na Miaka Hiyo Hiyo, Lakini Utawakuta Wenzako Wakiwa Na Miaka 85.
 
Anaitwa Mansa Musa, Alikuwa Mfalme Wa Mali (1312-1337). Ndiye Binadamu Aliyewahi Kuwa Na Utajiri Mkubwa Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani. kutokana Na Kumiliki Machimbo Mengi Ya Dhahabu. Utajiri Wake Ulikuwa Sawa Na Dola Za Kimarekani Bilioni $400 Kwa Thamani Ya Pesa Ya Sasa.
 
Back
Top Bottom