Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutokana na msimamo wake wa kupinga ubaguzi wa rangi uliokithiri nchini humo kwa wazungu kuwaona watu weusi hawastahili heshima ya ubinaadam Malcolm X alipata maadui wengi kiasi alipewa majina kama mchochezi na mpenda ghasia.
 
Mwaka 1946 akiwa na miaka 20 Malcolm x alipelekwa gerezani kwa kosa la wizi, akiwa gerezani alibadili dini na kuwa Muislamu ambapo kidogokidogo alianza kupanda daraja na kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa dini ya kiislam nchini humo.
 
Katika harakati zake za kupigania haki za weusi nchini Marekani, Malcolm alifanikiwa kukutana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama Keneth Kaunda wa Zambia, Gamal abdu Naser wa Misri, Julius Nyerere wa Tanzania, Kwame Nkrumah wa Ghana, Patrice Lumumba wa Congo, Ben Bella wa Algeria na Rais wa Cuba Fidel Castro ambae alihudhuria katika moja ya mikutano yake ya harakati za haki za binaadam
 
Hata Abdulrahman Babu aliwahi kuwa mgeni mualikwa katika moja ya mikutano ya Malcolm X alipotembelea nchini Marekani kama rafiki wa mapinduzi ya watu weusi duniani. Wakati huo Babu alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, na Babu ndie aliemuunganisha Malcolm X na Mwalimu Nyerere.
 
Siku ya tarehe 21 February, 1965 wakati akihutubia katika mkutano wa Afro-American Unity katika mji wa Manhattan Marekani mbele ya umati wa watu 400 alipigwa risasi kadhaa mwilini na kukimbizwa hospitali ya Columbia Presbyterian na kutangazwa amefariki saa 3:30 usiku muda mchache baada ya kukimbizwa hospitalini hapo.
 
Bila shaka kwa ufupi umemfahamu mkali huyu aliyetikisa ulimwengu katika harakati zake za kumtetea mtu mweusi na kupinga ubaguzi. Mpaka sasa amekuwa miongoni mwa 'icon' maarufu za wanaharakati wa kutetea haki za watu weusi duniani kama ilivyo kwa King Martin Luther.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…