Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KENYA: Kondakta wa daladala jijini Nairobi, Daniel Mwaura amepewa kiasi cha TZS 2.9 milioni, huku mkewe akiahidiwa kuhudumiwa bure katika Hospitali ya Nairobi wakati anajifungua, baada ya kuonyesha ukarimu kwa kurudisha TZS 600,000 alizookota ndani ya gari lake.
 
RWANDA: Kampuni ya Ujerumani ya kutengeneza magari, Volkswagen, wiki iliyopita imeingiza sokoni magari yake mapya ambayo kwa mara ya kwanza yameundwa kwenye kiwanda chake kipya kilichopo nchini humo.
Volkswagen imeanza kwa kuwekeza Dola za Marekani milioni 20 ktk kiwanda hicho.
 
udakutz_Siku mbili tangu alipoachiwa muigizaji Elizabeth Michael ’Lulu’, mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema ameumia na tangu alipopata taarifa hizo hajalala.

Akizungumza na MCL Digital leo mama Kanumba amesema, tangu alipopata tetesi za msanii huyo ametoka jela, amejikuta anakosa usingizi na kuumwa presha.

Ameongeza na kusema, kutokana na suala hilo, imemlazimu leo Jumatatu kwenda kwenye maombi kwa ajili ya afya yake hiyo.

Amesema, licha ya kuwa si yeye aliyemuhukumu, Lulu alipaswa kukaa hata mwaka mmoja ili roho yake iridhike lakini ndio hivyo: "Siku zote maskini hana haki." Hata hivyo, amewashukuru wote waliohusika kumtoa na kuongeza kuwa yote ni kwa sababu yeye hana pesa na anajua watu wataanza kumtusi mitandaoni kwa sababu hiyo lakini yote anamuachia Mungu.

Jeshi la Magereza kupitia Ofisa Habari wake, Lucas Mboje, limesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
 
Kenya inatarajia kuizindua satelaiti yake ya kwanza siku ya Ijumaa Mei 11, mwaka huu.
Satelaiti hiyo itatumika katika utabiri wa hali ya hewa pamoja na tafiti za kilimo.
Satelaiti hiyo imeundwa na wakandarasi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wakisaidiana na wa Japan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…