Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ilikuwa ngumu kwetu kucheza bila ya Lukaku dhidi ya timu ambayo ilikuwa inajilinda na wachezaji tisa. Unahitaji mchezaji ambaye anasumbua. Chelsea sio wajinga. Wanajua timu yetu bila ya Lukaku au Marouane Fellaini tunakuwa hatuna usumbufu katika mipira ya hewani kwahiyo waliweka watu wanane au tisa kwa ajili ya kudhibiti mipira ya hewani na walitawala.”
 
Ilikuwa ngumu kwetu kucheza bila ya Lukaku dhidi ya timu ambayo ilikuwa inajilinda na wachezaji tisa. Unahitaji mchezaji ambaye anasumbua. Chelsea sio wajinga. Wanajua timu yetu bila ya Lukaku au Marouane Fellaini tunakuwa hatuna usumbufu katika mipira ya hewani kwahiyo waliweka watu wanane au tisa kwa ajili ya kudhibiti mipira ya hewani na walitawala.”
 
Kila kipigo huwa kinaumiza lakini nakwenda nyumbani nikiwa na hisia kwamba tulijaribu kila tulivyoweza. Sina majuto.”

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka England alienda tofauti na Mourinho ambapo alimpongeza Kocha wa Chelsea, Antonio Conte kwa mbinu zake dhidi ya Mourinho ambazo ziliipa ubingwa wa FA Chelsea.
 
Haikufanya kazi kwa Man United lakini inabidi umpe sifa Conte. Timu yake ilikaa sana nyuma na ilinishangaza. Awali nilidhani Chelsea ndio ambao wangemiliki mpira na United wangefanya mashambulizi ya kushtukiza. Lakini Conte alijua hatari kubwa kwa United ilikuwa kasi yao eneo la mbele. Hakukuwa na njia yoyote kwa Sanchez na Rashford kukimbia. Unaweza kusema United walimiliki mpira taratibu,” alisema Scholes.
 
Scholes pia alimshambulia staa wa United, Alexis Sanchez akimtaka aonyeshe ubora wake huku pia akimpiga kijembe kiungo Mfaransa wa timu hiyo, Paul Pogba.

“Kiwango chake inabidi kiimarike. Hawawezi kwenda chini ya hapo. Nadhani katika mechi chache zijazo za msimu mpya itakuwa muhimu kwake. Anahitaji mashabiki wawe nyuma yake na waamini wataikamata Manchester City. Wanahitaji mchezaji mkubwa,” alisema Scholes.
 
Wana wachezaji wakubwa? Paul Pogba hawezi kuwapa ushindi kwa juhudi zake binafsi. Hazard anaweza kufanya hivyo. Alexis Sanchez hawezi, ameonyesha tangu Januari, walidhani angeweza, lakini kwa tulichoona mpaka sasa ni kwamba hawezi.”

“Wanahitaji wachezaji wa kufanya maajabu. Nadhani wana wachezaji wazuri lakini hawajawapata kama Hazard, (Cristiano) Ronaldo, (Lionel) Messi, na najua timu nyingi hazina wachezaji hao.

Leo tofauti ilikuwa Hazard. Tumeliona hilo katika mechi kubwa,” alimaliza.
 
DUH! West Ham United imemfanyia kitu mbaya sana Kocha David Moyes.

Jinsi ilivyomchinja, hata mwenyewe anashangaa. Ishu ipo hivi, Moyes alikuwa na uhakika wa kupewa muda zaidi wa kuinoa timu hiyo na alipewa mkataba mpya kwenye kikosi hicho cha London.
 
Lakini, mwenyewe akaremba na kuwaambia mabosi wa West Ham wasubiri msimu umalizike kwanza ndipo waketi chini kujadili malipo yatakavyokuwa, lakini sasa Wagonga Nyundo hao wa London wamemgeuzia kibao na kumtosa kama hawamfahamu vile.
 
Moyes alitua West Ham United, Novemba mwaka jana wakati alipopewa dili la muda tu kufuatia kuondolewa kwa Kocha Slaven Bilic na alifahamu ataendelea kubaki kwenye timu hiyo, kabla ya mambo kubadilika wiki iliyopita, alipoambiwa hakutakuwa na dili jipya tena hivyo, asepe zake tu.
 
West Ham sasa imeamua kumpa kazi aliyekuwa kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini na huenda akatua London muda wowote baada ya kuachana na klabu ya Hebei China Fortune aliyekuwa akiinoa huko kwenye Ligi Kuu China.
 
Watu wanapofikiri kuhusu ulimwengu basi wanafikiria nyota. Nyota ndizo zinazofanya sehemu kubwa ya yabisi, kiminika na hewa (matter) inayoonekana na ingawa nyota zote mbali na jua ziko katika umbali usiofikirika kutoka tulipo, bado tunaweza kuziona nyotamaelfu kwa maelfu kwa macho yetu wenyewe. Kuna maajabu mengi ya ukweli kuhusu nyota lakini nitaongelea machache yanayovutia na wengine wanaweza kuongezea ili tijifunze au kueleweshana pamoja.
 
1.Idadi ya nyota katika ulimwengu unaoonekana

Katika usiku wenye giza tororo katika maeneo ya vijijini au mbali na mji unaweza kujionea nyota zisizo na idadi lakini katika mazingira ya kawaida hapo unakuwa unaangalia nyota kama 2500 na si zaidi ya hapo. Hizo ni moja ya billioni 1/100,000,000 ya jumla ya nyota zilizo katika galaxi tuishiyo (MilkyWay).
 
Milky way ni moja ya galaxi kubwa sana katika universe na sisi tumebahatika kuwa ndani ya galaxi hii. Labda kidogo tuangalie kwa kifupi ukweliwa galaxi hii. Diameter (kipenyo) ya Milky Way kutoka upande mmoja mpaka mwingine ni umbali wa miaka laki moja (100,000) ya mwendo wa mwanga. Mwendo wa mwanga kwa mwaka ni jinsi mwanga unavyosafifi kwa mwaka mzima kutoka point moja mpaka nyingine. Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.
 
Hivyo mwaka mmoja wa kusafiri kwa mwanga (a light year) ni umbali wa kustaajabisha. Inaweza kuchukua miaka elfu kumi na nane kwa chombo chenye kasi zaidi cha anga kusafiri mwaka mmoja wa mwanga. Sasa hapa ku-cover distance ya kipenyo cha MilkyWay tunazungumzia umbali wa miaka 100,000 ya kusafiri kwa mwanga.
 
Hii pia ina maana unapochukua telescope ukafanikiwa kuziona nyota zilizoko upande mwengine wa mwisho wa galaxi, basi unaziona jinsi zilivyokuwa miaka 100,000 iliyopita, kwa sababu mwanga uliotoka kwenye nyota hizo miaka laki moja iliyopita ndio kwanza unatufikia. hii ni sawa pia kwamba kama kuna kiumbe katika upande mwingine wa galaxi na anaiangalia dunia kwa telescope basi ataiona dunia kama ilivyokuwa miaka 100,000 iliyopita.
 
Katika picha hiyo ya Milkyway galaxi unaweza kudhani mojawapo ya vidoti hivyo ni jua letu. Ukweli ni kwamba kama ukiikuza picha hiyo ifikie ukubwa wa saizi ya Dunia, bado ungehitaji microscope ili kuweza kuona kidoti cha mwanga wa jua letu. Hii ni kutokana na kwamba kama Milkyway galaxi ingepunguzwa iwe kama size ya Dunia, basi jua lingekuwa 1/50 ya millimita (kipenyo). Hii ni sawa na kidoti tusichoweza kukiona kwa macho.
 
Kwani kuna Galaxi ngapi?

Mwaka 1995, wanasayansi walichagua kajisehemu kadogo sana katika anga ambako kwa macho ya kawaida kalikuwa kanaonekana hakananyota yoyote wala mwanga wowote. pia kwa telescope ya kawaida kaeneo haka bado kalionesha hakana kitu chochote yani ni giza tu. Eneo hili dogo ambalo lilionekana tupu ni kama vile eneo linaloweza kuzibwa na mpira wa tenis ukiwa juu yako kwa mita mia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…