Mtu anaweza kufikiria zaidi kuhusu tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa lishe, lakini kilichobainika kutoka kwa utafiti huu wa China ni kwamba kula angalau yai moja kwa siku hakuongezi hatari ya kuugua maradhi ya moyo, na badala yake kuna faida," anasema Prof Nita Forouhi, wa Chuo Kikuu cha Cambridge.
Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la masuala ya moyo la Heart, ulifanywa baada ya miaka mingi ya watu kuonyesha dhidi ya ulaji mayai.
Watu walikuwa wakitahadharishwa kwamba kula mayai kunaweza kuwasababisha kuambukizwa viini vya salmonella na pia kwamba yana kiwango cha juu cha cholesterol.