Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wewe unapenda kufanya makosa? Mimi binafsi sipendi kufanya makosa.

Ingawa watu wengi wamekuwa wakijaribu kujitahidi kuepuka makosa; bado wamejikuta wakiendelea kufanya makosa.

Ni wazi kuwa makosa hayaepukiki kwenye maisha ya kila siku ya binadamu. Kutokana na sababu za kibinadamu, maamuzi na matendo tunayoyafanya yana mapungufu mbalimbali; hivyo haiwezekani kuepuka makosa.
 
Kama haiwezekani kuepuka makosa sasa tunafanyaje? Jibu ni wazi kabisa kuwa tunajifunza kutokana na makosa hayo ili tuyaepuke au tuboreshe mambo mbalimbali mbeleni.

“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo.”
Bill Ackman
Karibu nikufahamishe mambo 25 ambayo unaweza kujifunza kutokana na makosa mbalimbali unayoyafanya kila mara maishani mwako.
 
2. Hutufundisha maana ya mafanikio

Pasipo shaka, mafanikio siyo mteremko au ukamilifu. Mafanikio ni kujifunza kutokana na makosa na kuepuka kuyarudia tena mbeleni. Kupitia makosa tunaweza kujifunza tufanye nini ili tufanikiwe katika lile tunalolifanya.
 
3. Hutufundisha kuomba msaada na ushauri

Tunapofanya makosa, mara nyingi tunatambua kuwa tunahitaji watu wakutusaidia kuyarekebisha au kutupa ushauri. Kabla ya kufanya kosa ambalo limekuletea matatizo, unaweza kufikiri unajitosheleza au hauhitaji msaada wowote.
 
4. Hutuwezesha kufahamu mambo ya msingi

Inawezekana kosa limetokea kutokana na kufanya au kuzingatia jambo ambalo siyo la msingi. Hivyo kwa njia ya kosa hilo utaweza kubaini mambo ya msingi na yasiyo ya msingi.
 
5. Hutufundisha umuhimu wa wengine

Inawezekana umekosea kwa sababu umepuuza nafasi ya watu wengine katika maamuzi au kile unachokifanya. Kwa sababu hii basi utakuwa umefahamu umuhimu wa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…