Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

10. Hutuwezesha kubaini nafasi ya chaguzi nyingine

Inawezekana kuna uchaguzi fulani uliupuuzia au hukufahamu umuhimu na ubora wake. Baada ya kukosea katika uchaguazi ulio uchagua utabaini kuwa uchaguzi ulioupuuzia una nafasi kubwa.
 
13. Hutufundisha unyenyekevu

Mtu anapokosea mara nyingi huwa mpole na mnyenyekevu; hii ni kutokana na kutambua udhaifu au mapungufu aliyoyafanya. Hivyo makosa ni njia bora kabisa inayoweza kutufundisha na kutufanya kuwa wanyenyekevu.
 
14. Hutufundisha muda sahihi wa kufanya mambo

Makosa mengine hutokea kwa sababu maamuzi au jambo limefanywa nje ya wakati. Kwa kupitia kosa, tunaweza kujifunza ni wakati gani stahiki tunapaswa kufanya jambo au maamuzi fulani.
 
15. Kutuonyesha matatizo kwenye mahusiano

Matatizo kwenye mahusiano hubainika hasa pale mtu mmoja anapomkosea mwingine.

Kila upande utajitahidi kutaja na kuonyesha matatizo yaliyopo kwenye mahusiano husika ili kuficha kosa; hivyo kwa njia hii makosa yatawezesha kubaini matatizo yaliyoko kwenye mahusiano.
 
19. Hutufundisha kuwa mafanikio siyo kila kitu

Ikiwa unafanikiwa kila mara, ni rahisi kujiaminisha kuwa mafanikio ndiyo kila kitu kwenye maisha. Lakini utakapofanya makosa na kushindwa utabaini kuwa bado maisha yanendelea kama kawaida.
 
23. Kujifunza kutumia pesa vyema

Mara nyingi tunakosea kutokana na kushindwa kutumia pesa vyema. Tunapokuwa kwenye matatizo kutokana na makosa ya matumizi mabaya ya pesa; tutajifunza kuwa wakati mwingine inatupasa kutumia pesa vyema.
 
25. Tunajifunza marafiki sahihi ni wapi

Ikiwa utafanya kosa kutokana na aina ya marafiki ulio nao, ni wazi kuwa kosa hilo litakufundisha umuhimu wakutazama aina za watu au marafiki unaoshirikiana nao. Marafiki bora watakutia moyo na kukuhamasisha kuendelea mbele ili kutimiza malengo yako na siyo kukuzamisha.
 
Back
Top Bottom