UTAFITI: Watu wanaochelewa kulala wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kuliko wale wanaowahi kulala - Msingi wa utafiti huo ni kwamba watu wanaolala muda mzuri na kuamka mapema wanaweza kuishi muda mrefu ukilinganisha na wale ambao wanachelewa kulala ambao wakati mwingine wanaamka mapema wakiwa na uchovu mwingi - Matokeo ya utafiti huo yamechambua sampuli ya watu laki 5 wenye umri wa miaka 30 hadi 73 ambao walifuatiliwa tabia za ulalaji wao kwa zaidi ya miaka 6 na nusu - Watafiti walibaini kuwa watu ambao walikuwa wanachelewa kulala walikuwa na hatari kwa asilimia 10 kufa mapema katika kipindi cha utafiti kuliko wale ambao wanalala mapema na kuamka mapema"
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.