Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

18. Unaweza kuishi siku 30 bila chakula

Inaelezwa kuwa binadamu anaweza kuishi siku 30 bila chakula; siku 3 bila maji; dakika tatu bila oksijeni. Je ulilifahamu hili kuwa unaweza kunywa maji tu bila kula na ukaishi siku thelathini?
 
19. Unaweza kukaa bila kulala kwa siku 11

Rekodi ya dunia ya mtu aliayeweza kukaa muda mrefu zaidi bila kulala iliwekwa na Randy Gardner ambaye alikaa siku 11 pekee. Inaelezwa kuwa ukikaa zaidi ya hapa utaanza kupata matatizo ya kiakili na kisaikolojia.
 
20. Mawimbi kwenye mfumo wa fahamu husafiri kwa kasi ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa)

Inaelezwa kuwa unapomgusa mtu au kitu kinapomgusa mtu, tarifa za tendo hilo husafiri kwa kasi kubwa ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa) kuelekea kwenye ubongo.
 
23. Ubongo unaweza kutunza kiasi kikubwa cha kumbukumbu.

Kwa kipindi cha maisha ya binadamu yote, ubongo wake unaweza kutunza biti za data zipatazo milioni bilioni moja. Milioni bilioni moja? Ndiyo, milioni bilioni moja na zaidi.
 
24. Moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili

Nini? Ndiyo, moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili ikiwa tu utapata oksijeni. Moyo umeumbwa kwa namna ambayo unazalisha mawimbi yake ya umeme wenyewe yanayowezesha misuli yake kusukuma damu. Hii ndiyo sababu wataalamu wa tiba wanaweza kuutoa moyo na kuurudisha tena bila shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…