Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema watu watano waliotoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli wameuawa na wananchi baada ya kurejea katika matendo maovu.

Sirro aliyewataka wanaoachiwa huru kwa msamaha wa rais kutorejea katika matendo hayo, ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 24, 2018 mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kisasa vya Mburahati, Kiluvya-Gogoni na Mbweni vilivyozinduliwa leo.
 
Nia ya Rais Magufuli kuwapa msamaha ilikuwa njema lakini kuna baadhi ya watu wameitumia vibaya fursa hiyo na hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi,” amesema.

“Ukitoka gerezani kwa msamaha, maana yake umerekebisha mwenendo wako na wananchi wanatarajia uwe hivyo, lakini kama ukifanya vinginevyo Serikali isilaumiwe.”

Akizungumzia utendaji wa jeshi hilo, Sirro amesema tangu ashike madaraka hayo polisi wamewapeleka askari 1,267 kwenye mafunzo ya medani za kivita na wako imara.
 
Pia tumepeleka askari wa upelelezi zaidi ya 1,000 kwenye mafunzo ya ujuzi na ustadi wa kupeleleza kesi mbalimbali. Baada ya kuwapa mafunzo haya, tunataka kesi za kawaida upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi sita” amesema na kubainisha kuwa kesi kubwa upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi 12.

Pia, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia Sh10 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari, kutoa kibali cha ajira kwa askari wapya 1,500 na kuwaruhusu wawapandishe vyeo askari wenye kustahili kuanzia cheo cha koplo hadi naibu kamishna wa polisi (DCP).
 
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limesema siku za kumkamata mtuhumiwa wa ujambazi anayeteka watu na kuwapora kwa kutumia bunduki bandia na kisu, zinahesabika.

Limesema kuwa mtuhumiwa huyo amenusurika kukamatwa mara mbili baada ya kuwekewa mtego na polisi.

Akizungumza leo Alhamisi Mei 24, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amesema mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halisi halijulikani, anafanya uhalifu kwa kuteka watu na kuwapora mali zao katika barabara ya Kisili-Buhigwe kwenye pori la Kwitanga.
 
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limesema siku za kumkamata mtuhumiwa wa ujambazi anayeteka watu na kuwapora kwa kutumia bunduki bandia na kisu, zinahesabika.

Limesema kuwa mtuhumiwa huyo amenusurika kukamatwa mara mbili baada ya kuwekewa mtego na polisi.

Akizungumza leo Alhamisi Mei 24, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amesema mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halisi halijulikani, anafanya uhalifu kwa kuteka watu na kuwapora mali zao katika barabara ya Kisili-Buhigwe kwenye pori la Kwitanga.
 
Pori hilo lipo katikati ya kijiji cha Mahembe na Gereza la Kwitanga katika wilaya ya Kigoma.

"Tunaendelea kumsaka na polisi wamemkurupusha mara mbili ikabidi adondoshe bunduki yake chini, kumbe ni ya bandia na ndio anayotumia kupora watu," amesema Ottieno.

“Bunduki hizo bandia zimechongwa kwa kutumia mbao kiasi kwamba mtu akiitazama kwa mbali bila kuichunguza hawezi kutambua kama ni bandia.”
 
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kupora watu wanaopita barabarani wakiwa kwenye magari, pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu ambapo hunyang'anya simu za mkononi na fedha.

Ottieno ameomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wa dhati kwa askari ili iwe rahisi kumkamata jambazi huyo.
 
Unatoka gerezani kwa msamaha wa rais halafu unaishia kuuawa na wanachi wenye hasira kali. Nice !!!
 
Sina uhakika kama Ivanka atapona ktk mawindo ya Rooney
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…