Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je unalifahamu jengo la Burj Khalifa lililoko Dubai? Burj Khalifa ni jengo refu zaidi duniani linalodhihirisha uwezo mkubwa wa wahandisi majengo wa karne ya 21. Unapozungumzia urefu wake au kutazama muundo wake, kwa hakika jengo hili litakushangaza; jengo hili liligharimu takriban dola bilioni 1.5 za Kimarekani kulijenga. Pamoja na kuwa ni jengo refu zaidi duniani, jengo hili limevunja rekodi nyingine kadha wa kadha zilizokuwa zimewekwa na majengo mengine.
 
Naamini unapenda kulifahamu zaidi ili kuongeza maarifa yako. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujulishe mambo 20 usiyoyajua kuhusu jengo hili la Burj Khalifa.

Burj Khalifa ni jengo refu zaidi lililotengenezwa na binadamu duniani, lina urefu wa futi 2,723 au mita 829.8 kutoka kwenye kilele chake hadi ardhini. Hivyo kulifanya jengo hili kuwa refu zaidi huko Dubai, Umoja wa falme za Kiarabu, Mashariki ya Kati na Duniani. Jengo hili ni refu mara 3 kuliko mnara wa Eiffel huko Ufaransa na mara mbili zaidi kuliko Dola State Building.
 
Jengo hili awali lilikusudiwa kuitwa Burj Dubai, lakini baadaye likaitwa Burj Khalifa kumuenzi Sheik Khalifa bin Zayed al-Nahayan aliyekuwa kiongozi wa falme za Kiarabu
 
Eneo lake la kutazamia mandhari (observatory deck) liko kwenye muinuko wa futi 1483 au mita 452.1 kutoka chini. Hili ni eneo ambalo watu husimama na kutazama mji au mazingira kwa chini. Hii ni kusema kuwa eneo hili liko kwenye mwinuko wa umbali wa takriban urefu wa viwanja vinne na nusu vya mpira wa miguu.
 
Jengo hili lina ghorofa 163 zilizoko juu ya uso wa ardhi na moja iliyoko chini ya uso wa ardhi.
Ujenzi wa jengo hili ulipendekezwa mwaka 2003, likaanza kujengwa mwaka 2004 na kisha kukamilika mnamo mwaka 2010.
 
Jengo hili limeshikilia rekodi mbalimbali za dunia kama vile “jengo refu zaidi duniani”, “jengo lenye lifti inayosafiri kwa kasi na kwa urefu mkubwa zaidi”, “eneo la kutazamia lililoko juu zaidi (observatory deck)” na “jengo linalokaliwa na watu wengi zaidi”. Hata hivyo rekodi ya eneo la kutazamia lililoko juu zaidi imeshachukuliwa na jengo la Canton Tower lililofunguliwa mwaka 2011.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…