Mtakatifu mtakatifu, asante Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku nyingine tena, siku kuu, j'pili takatifu ya mwisho wa mwezi..
Tunasema asante Baba kwa maana peke yetu hatuwezi pasipo mkono wako wa REHEMA.
Nawakabidhi mikononi mwako wapendwa hawa,wana likes, kapate kuwalinda na kuwatunza BWANA, bariki afya zao, familia zao,bariki kazi za mikono yao, kawakumbuke wale wote waliokata tamaa ya afya zao, maisha yao..Kawabariki wakapate kuwa na mahusiano mazuri kazini,na hata katika jamii zao kwa ujumla, wakakukumbuke wewe wangali hai BWANA..
Namkabidhi mikononi mwako mpenzi wangu, rafiki yangu, msiri wangu,roho yangu (****) kapate kumpa macho ya rohoni Bwana, akujue wewe zaidi, akupende, akutii na kukutumainia siku zote.
Namfunika kwa DAMU ya mwanao YESU KRISTO umuepushe na tamaa na vishawishi vya kila namna, umuepushie mbali na mabaya yote, simama BWANA, ulinde mahusiano yetu na utuganye kuwa IMARA wenye kusimama katika IMANI inayokupendeza JEHOVA..[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
**Mkumbushe NAMPENDA SANA.**
Nawakabidhi mikononi mwako wale wote walio katika mwezi mtukufu, funga yao ikawe funga ya kweli, wakupendeze wewe Baba.
Nasema asante kwa FURAHA na AMANI unayoendelea kutupatia miongoni mwetu.
Naombea UPENDO na UTU WEMA ukapate kudumu miongoni mwetu Baba..
Tufanye tuwe vichwa siku zote BWANA..Daima tukapate kujiinamisha kwako kwa unyenyekevu..
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]