Jaribu kukumbuka umbo na rangi ya Nyoka:
Kufahamu namna ambavyo Nyoka anavyofanana kunasaidia wakati wa matibabu baadaye, lakini usijaribu kumshika kwa kuwa utakuwa hatarini hata akaleta madhara kwa mtu mwingine.
Ondoka eneo la hatari
Kama uko mwenyewe mbali na msaada, jambo la kwanza ni kwenda eneo lenye usalama.Tafuta eneo ambalo utaomba msaada.Kama uko na watu wengine wacha wakubebe kama inawezekana,ili kupunguza kiasi cha sumu kutembea mwilini,wataalam wanaeleza.
Usifyonze sumu kutoka kwenye jeraha
Sumu huingia ndani kabisa kwenye eneo la kati ya ngozi na misuli na husambaa mara moja (ndani ya dakika moja).Hivyo haiwezekani kuondoa sumu kwa kunyonya kwani itazidisha maumivu na uharibifu zaidi pasipo na ulazima.
Ondoa vitu vilivyovaliwa sehemu iliyoathiriwa
Vua vitu kama pete au nguo zinazobana katika eneo ambalo madhara yametokea kama mkononi kwa sababu vinaweza kusababisha damu kutotembea vizuri.