Hata hivyo huenda Bale asihamie Manchester City huku mabingwa hao wa Ligi ya Primia wakionekana kutokuwa na haja ya kusaini mkataba na mchezaji huyo wa kiungo cha kati. (Guardian)
Manchester United wamewasilisha ombi la thamani ya Euro milioni £96m la kumnunua mchezaji wa timu ya Lazio anayecheza safu ya kati Mserbia Sergej Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)
Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya Lyon na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 24, anasema ''hajakaribia'' kuhamia Liverpool na atachukua muda kufikiria juu ya hali yake . (Telefoot via Sky Sports)
Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya Lyon na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 24, anasema ''hajakaribia'' kuhamia Liverpool na atachukua muda kufikiria juu ya hali yake . (Telefoot via Sky Sports)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Paul Pogba amedai kurejea Juventus. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ufaransa alikuwa miaka minne na championi ya Serie A baada ya kuhamia Italia kutoka Old Trafford mwaka 2012. (Tuttosport via Express)
Real Betis wameanza mazungumzo na ManchesterUnited kuhusiana na uwezekano wa Mbrazil Andreas Pereira, mwenye umri wa miaka 22 anayecheza safu ya kati kucheza kwa deni katika kikosi cha uhispania katika timu za Granada na Valencia. (Mirror)
Mshambuliaji wa Roma Edin Dzeko sanasema kuwa aliambiwa aikatae Chelseawakati wa msimu wa kuhama uliopita. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Bosnia mwenye umri wa miaka 32, aliongeza kuwa atakua tayari kwa uhamisho kutoka katika mji mkuu wa Italia msimu huu . (Face TV via Sun)
Inter Milan wamepanga kukutana na mshambuliaji Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 25, katika kipindi cha wiki moja ijayo kujadili mkataba mpya kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (Football Italia)
Liverpool iko tayari kurefusha zaidi mkataba wa mchezaji wa England wa safu ya kati - nyuma Joe Gomez kuongeza mkataba , licha ya kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 bado ana miaka minne yya kuendelea kutumikia mkataba wake katika Anfield. (Sun)
mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Scott McTominay, mwenye umri wa miaka 21, ameahidi kuchezea Uskochi siku zijazo , akisema hakuna "nafasi" kwake ya kuichezea England . (Mail)