Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Leo hii ndiyo nimeusikiliza wimbo wao wa Melanin kwa mara ya kwanza baada ya kuletewa na mtu.
Nimejishangaa sana kwanini hawa jamaa hawapigiwi promo inavyotakiwa aisee....
[emoji23][emoji23][emoji23]Imebidi tu nicheke kwanza
Hapo ndo kwenye shida sasa, ila wanajitahidi kujitangaza
Mwanaume effort [emoji123][emoji23]
 
Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel.
Maafisa wa uhamiaji wameiambia BBC kuwa alihojiwa wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Israel mjini Moscow. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.
Mzozo huo ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal.
Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa.
 
Viza yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'.
Kucheleweshwa kwa utoaji wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza.
Bwn Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United 1-0.
 
Vyombo vya habari vya Israeli vinasema kuwa tayari amepewa kitambulisho cha uraia nchini Israeli chini ya sheria ya kurudi nyumbani, ambayo inawawezesha wayahudi popote pale walipo duniani kurudi na kuwa raia wa Israel.
Gazeti la The Times nchini Israeli limeandika kuwa Bw Abramovich aliwasili Israeli Jumatatu na kwamba amehamia nchini humo.
 
Ni mtu ambaye amekuwa akiitembelea Israeli mara kwa mara na alinunua hoteli mjini Tel Aviv mnamo mwaka 2015 ambayo inasemekana ameigeuza kuwa makazi yake.
Wamiliki wa pasipoti ya Israeli wanaruhusiwa kuingia Uingereza kwa siku chake bila kuwa na visa.
Bw Abramovich ana utajiri wa thamani ya dola bilioni $11.5bn (£8.6bn), kulingana na jarida la Forbes.
Kuhamia kwake Israel kunaweza kumsaidia kifedha kwa sababu kama raia mpya wa Israeli ataweza kuondolewa ushuru unaolipwa na wawekezaji wa kigeni kwa muda wa miaka 10.
 
Ni miongoni mwa watu tajiri zaidi Urusi, aliinunua klabu ya Chelsea FC mwaka 2
Inadaiwa aliuza midoli (wanasesere) kabla ya kuwekeza katika mafuta miaka ya 1990 baada ya kusambaratika kwa uliokuwa Muungano wa Usovieti
 
Bw Abramovich alikuwa wakati mmoja mshirika wa kibiashara wa tajiri wa zamani marehemu Boris Berezovky, rafiki wa rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin
Wakosoaji wanasema wafanyabiashara hao wawili walitumia ukaribu wao na ikulu ya Kremlin kujipatia umiliki wa mashirika mengi ya serikali kwa 'bei ya kutupa'
 
Mchezji soka wa England Raheem Sterling ametetea tattoo yake mpya ya bunduki kwenye mguu wake akisema ''ina maana kubwa sana" akimaanisha ina uhusiano na mahrehemu baba yake .
Wanaharakati wanaopinga silaha wamemkosoa mshambuliaji huyo wa Manchester City baada ya kuushirikisha umma picha yake ya tattoo ya silaha hiyo aina ya M16 kwenye mguu wake.
Picha hiyo imetajwa kama "isiyokubalika kabisa" na "inayoudhi".
Lakini Sterling amesema ni ishara ya kiapo alichoapa kwamba "hatawahi kushika bunduki" baada ya baba yake kupigwa risasi alipokuwa mvulana mdogo.
Sterling, mwenye umri wa miaka 23, ambaye atakwenda Urusi msimu huu kam sehemu ya kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dinia , alifichua tattoo yake kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa anafanya mazoezi na wenzake katika St George's Park.
 
Lucy Cope, muasisi wa kikundi cha Mama wanaopinga bunduki (Mothers Against Guns) baada ya mwanae kupigwa risasi na kuuawa mwaka 2012, amesema Sterling hapaswi kuichezea England mpaka atakapoondoa tattoo.
 
Akizungumza na gazeti la Sun alisema: " tatoo hii inaudhi. Raheem anapaswa kuibika. Haikubaliki kabisa.
"Tunadai aondoe ama aifiche tattoo yake na mchoro mwingine .
"Kama atakataa kutusikia basi aondoshwe kwenye timu ya England. Anapaswa kuwa mfano wa kuigwa , lakini badala yake ameamua kuchagua kujipamba na bunduki ."
Sterling, alijiungana timu ya City kutoka Liverpool kwa pauni 49 mwezi wa Julai 2015, alijibu ukosoaji huo kwenye Instagram Jumatatu jioni.
 
Mchezaji wa zamani wa England ambaye kwa sasa ni mchanganuzi wa masuala ya michezo Gary Lineker amesema kuwa ''Sterling ni mchezaji hatari wa soka mwenye maadili mazuri ya kazi'', na akasema namna gazeti la Sun lilivyomuelezea "inaudhi".
 
Chengaaa[emoji23]
IMG-20180529-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom