Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu, Mariamu Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu mahakamani baada ya kushindwa kutoa nyaraka zinazothibitisha binti yake ameshindwa kufika kutokana na kuwepo nchini India kwa ajili ya matibabu. Tukio hilo limetokea leo , katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema, ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa na yeye kutoa nyaraka za kusafiria badala ya zile za matibabu. Wakati Wakili wa Serikali, Constantine Kakula akidai mahakamani kwamba kesi ilitakiwa kusikilizwa ushahidi wa upande wa utetezi lakini mshtakiwa wa kwanza, Wema hayupo, mama Wema alidai msanii huyo ni mgonjwa yuko nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na akawasilisha nyaraka alizodai kwamba zinathibitisha kuwa mgonjwa yuko kwenye matibabu. Hata hivyo nyaraka hizo baada ya kukabidhi nyaraka hizo kwa Wakili wa Serikali, Kakula alizikagua na kudai kwamba ni nyaraka za kusafiria ambapo na kumuomba mama Wema amuonyeshe mahali ilikoeleza kuhusu matibabu. Hata hivyo Mama huyo alishindwa kuzielezea na kudai kwamba Wakili wa msanii huyo Albert Msando atakwenda kuzielezea. Kes hiyo imeghairishwa hadi Juni 13, mwaka huu ambapo mshtakiwa ametakiwa afike mahakamani na uthibitisho wa matibabu na kama hakutakuwa na uthibitisho, mahakama itatoa amri nyingine yoyote inayofaa.
 
GWIJI wa Chelsea, Frank Lampard amesema beki wa Real Madrid, Sergio Ramos hapaswi kulaumiwa hata chembe juu ya suala la Mohamed Salah kuumia bega katika mechi ya fainali iliyokutanisha timu zao juzi Jumamosi usiku kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Kiev, Ukraine.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Real Madrid kuichapa Liverpool 3-1, Salah alitoka uwanjani mapema sana akiwa ameumia bega baada ya kuchuana na Ramos, aliyeonekana kumbana mkono kabla ya kumwangukia wote walipofika chini.
 
Mashabiki wengi wa Liverpool walielekeza hasira zao kwa Ramos kutokana na maumivu ya Salah, lakini Lampard ambaye kwa sasa ni mchambuzi alisema nahodha huyo wa Los Blancos hastahili lawama za aina yoyote ile.

Lampard alipoulizwa kama anadhani Ramos alaumiwe kwa kilichotokea, kiungo huyo wa zamani wa England, alisema: “Hapana, sidhani kama kuna kitu kama hicho. Kilichotokea nadhani ni bahati mbaya tu.”
 
Baadaye, Ramos alionyeshwa akionekana anacheka na mmoja wa waamuzi wasaidizi wakati Salah akiwa anatolewa nje huku akimwaga machozi, lakini Rio Ferdinand alisema tukio la kucheka na lile la kuumia kwa Salah ni mambo mawili tofauti. Rio, aliyewahi kucheza Manchester United alisema: “Siwezi kuvihusisha vitu hivyo viwili. Nadhani alifanya kazi yake vizuri ya kukaba na sidhani kama alidhamiria kumuumiza Salah.”
 
Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali.
Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
Mangenisium
Mangnese
Potasium
Copper
Vitamini B6
Hii ikiwa katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa wataalamu kutengeneza tangawizi ni tiba tosha kwa magonjwa ya ngozi
 
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.

-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
 
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.

-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…