Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mfumo endeshi huo kutoka Google kwa sasa umeliteka soko la mifumo endeshi ya simu na kuwaacha mbali sana wapinzani wake kama iOS, Windows, Blackberry na Symbian.Wengi tunaotumia vifaa vinavyotumia mfumo endeshi huu wa Google lakini kuna baadhi ya vitu hatuvifahamu kabisa. Hii ndo orodha ya mambo kumi ya kustaajabisha yanayohusiana na mfumo endeshi huu.
 
1. Android haikugunduliwa na Google

Mfumo endeshi wa android uligunduliwa na Andy Rubin, Chris White, Nick Sears na Rich Miner kipindi hicho ikiwa inafahamika kama Android Inc mwaka 2013. Baadae Android ilinunuliwa na Google ambayo iliendelea kuumiliki mfumo endeshi huo mpaka sasa. Google walinunua mfumo endeshi huo kutoka kwa Android Inc August 2005 kwa dau la $50 milioni.
 
2. Google waliachia Android rasmi mwaka 2007

Mfumo endeshi wa Android uliachiwa rasmi na kampuni ya Google mwaka 2007 na kuanza kutumika katika smartphones na kamera. Hapo awali mfumo endeshi huo ulitengenezwa maalumu kwa ajili ya kamera.
 
3. Android ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kamera

Android kwa mara ya kwanza ilitengenezwa kwa ajili ya smartcameras, ila google waliona ubora wa mfumo endeshi huo katika simu na kuamua kuamishia katika simu na kuleta mapinduzi makubwa sana katika soko.
 
3. Android ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kamera

Android kwa mara ya kwanza ilitengenezwa kwa ajili ya smartcameras, ila google waliona ubora wa mfumo endeshi huo katika simu na kuamua kuamishia katika simu na kuleta mapinduzi makubwa sana katika soko.
 
4. HTC Dream ni simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android

Simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android ilikuwa ni HTC Dream ambayo iliachiwa rasmi mwaka 2008 na kampuni ya HTC. Simu hiyo ilianza kwa kutumia toleo la android 1.0 na iliboreshwa mpaka kufikia toleo la android 1.6. Hapo mwanzo android ilipigwa madongo sana kuwa mfumo endeshi uliokosa mwingiliano mzuri na mtumiaji, japo baadae maoni hayo yalibadilika na kuiona android kama inaleta mapinduzi katika soko.
 
5. Android inatumika na zaidi ya watu bilioni moja duniani kote

Makamu wa Rais wa Google katika kitengo cha Android bwana Sundar Pichai, alitangaza kuwa kwa sasa mfumo endeshi wa android unatumika na zaidi ya vifaa bilioni 1 duniani kote katika nchi zaidi ya 190.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…