Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuvuja kwa mafuta

Ikiwa gari litavuja mafuta ni rahisi sana kuwaka moto. Kumbuka mafuta ya gari pamoja na mafuta lainishi (oil) ni rahisi sana kushika moto.

Tafiti mbalimbali za ajali zimebaini kuwa kuvuja kwa mafuta ni chanzo kikubwa cha magari kuwaka moto.
 
Moto uliowazi (naked flame)

Kama ambavyo moto ulio wazi ni hatari kwenye nyumba, ndivyo pia ilivyo kwenye gari. Kuwasha vitu kama vile sigara ndani ya gari kunaweza kusababisha ajali ya moto.

Ni muhimu kuepuka matumizi ya sigara au kubeba vitu vinavyoshika moto kirahisi ndani ya gari.
 
Hitilafu ya umeme

Gari lina mfumo wake wa umeme ambao unatakiwa uwe salama na ufanye kazi jinsi ipasavyo. Mfumo wa umeme unapokuwa na hitilafu, unaweza kusababisha cheche za moto na kusababisha gari kuwaka moto.
 
Ni muhimu kuhakikisha unatafuta mtaalamu wa magari akague na kurekebisha mfumo wa umeme wa gari lako kila mara. Pia ni muhimu kutumia vifa bora vya mfumo wa umeme wa gari, kwani vifaa duni vinaweza kusababisha moto.
 
Moto uliowazi (naked flame)

Kama ambavyo moto ulio wazi ni hatari kwenye nyumba, ndivyo pia ilivyo kwenye gari. Kuwasha vitu kama vile sigara ndani ya gari kunaweza kusababisha ajali ya moto.

Ni muhimu kuepuka matumizi ya sigara au kubeba vitu vinavyoshika moto kirahisi ndani ya gari.
 
Gari halitakiwi lipate moto kupita kiasi. Ikiwa sehemu za gari zitapata moto kupita kiasi zinaweza kuyeyuka au kuwaka moto.

Inashauriwa kuhakikisha mfumo wa kupooza gari uko katika hali nzuri. Pia ni muhimu kupumzisha ghari mara kwa mara wakati wa safari ndefu ili lipoe.
 
Ajali

Msuguano unaweza kusababisha moto. Gari linapogongana na gari jingine au kugonga kitu kingine, linaweza kuzalisha cheche ambazo zitasababisha gari lishike moto.

Hivyo ni vyema kuzingatia kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali.
 
[emoji23]
IMG_20180531_221227_959.jpg
 
Hitilafu ya kimuundo

Kuna wakati matatizo ya kimuundo ya gari yanaweza kusababisha gari kuwaka moto. Hata hivyo, kutokana na matatizo ya kimuundo kuhusiana zaidi na watengenezaji, tatizo la kimuundo linapobainika hurekebishwa mara moja na watengenezaji.
 
Back
Top Bottom