Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matengenezo duni

Kama jinsi ambavyo umekwisha kuona kwenye hoja zilizotangulia hapo juu, ni muhimu sana kuzingatia swala la matengenezo. Mifumo ya gari kwa ujumla inahitaji matengenezo sahihi na kwa wakati.
 
Kwa mfano ikiwa hutozingatia matengenezo ya magurudumu, yanaweza kupasuka au kuwaka moto. Ni muhimu pia kuhakikisha mafuta lainishi (oil) yapo kwa kiwango kinachotakiwa ili kuepusha msuguano wa vyuma unaoweza kusababisha moto.
 
Vifaa vya nyongeza

Watu wengi hupenda kuongeza vifaa mbalimbali kwenye magari yao tofauti na vile vilivyotoka kiwandani pamoja na gari. Vifa hivi huweza kuwa taa, redio, mifumo ya ulinzi, n.k. Vifaa hivi vya nyongeza vingi havina ubora na havifungwi na wataalamu.
 
Tahadhari kabla ya hatari ni muhimu. Ni wazi kuwa ajali nyingi za magari kuwaka moto kwa sehemu kubwa huchangiwa na mambo yaliyoelezwa hapo juu. Ni muhimu tena sana kuzingatia matengenezo sahihi pamoja na kanuni muhimu za matumizi ya vyombo vya usafiri ili kuepusha ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…