Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp.
Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata Jumatano.
Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na $0.05 ( £0.04) kila siku.
Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa 1% ya thamani yake.
 
Rais Yoweri Museveni alikaririwa na vyombo vya habari nchini Uganda mwezi uliopita akisema kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa zaidi kwa taarifa za "udaku".
Wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai ya rais.
"Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa watu kujieleza ," Mwana Blogi Rosebell kagumile aliliambia shirika la habari la Reuters.
 
Takriban wabunge watatu wamekosoa sheria hizi mpya na kuzitaja kama "utozaji wa kodi mara dufu ", kulinga na gazeti binafsi Daily Monitor.
Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi, almaarufu Bobi Wine - pamoja na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon - wamesema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki
 
Mbunge mwingine , Patrick Nsamba wa chama tawala , amesema kuwa ushuru huo utawaumiza maskini zaidi
Ni rahisi sana kwa mbunge kusema asilimia 1% ni kiasi kidogo cha lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza sana
Kuna mkanganyiko kuhusu namna ushuru huo mpya kwa mitandao ya kijamii utakavyotekelezwa.
 
Waganda wanatumia mitandao ya kijamii kusambaza kauli zao za kutoafikiana na ushuru huo mpya ambao umepitishwa kufuatia ombi la rais Yoweri Museveni.
Katika barua yake kwa waziri wa fedha, Bwn. Museveni alisisitiza kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwasababu inachochea taarifa za udaku
 
Lakini alidai kuwa huduma ya data za intaneti haipaswi kuwekewa ushuru, kwa sababu manufaa yake ya kielimu.
Wataalam pamoja na mtoaji mmoja wa huduma za Intaneti wameelezea hofu yao juu ya namna ushuru wa mitandao ya kijamii na mamilioni ya Waganda kwa kutumia sim-kadi
Serikali inahangai kuhakikisha simu kai zote zinasajiliwa.
Mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu ya kisiasa nchini Uganda kwa chama tawala na upinzani.
Huduma ya mitandao hiyo ilifungwa wakati wa uchaguzi wa 2016.
 
wa Donald Trump kujadili uwezekano wa msamaha kwa mama mzee na bibi mwenye umri wa miaka 63 ambaye anatumikia kifungo cha maisha jela.
Alice Marie Johnson amekuwa gerezani kwa zaidi ya miongo kadhaa baada ya kupatikana na hatia ya matumizi ya dawa za kulevya kwa mara ya kwanza.
 
Mkwe wa rais Trump Jared Kushner amekuwa pia akizungumza na Bi Kardashian West juu ya kesi hiyo kwa miezi kadhaa.
Binti yake Johnson ameithibitishia BBCNews kwamba mkutano huo umefanyika.
Baadae Trump alituma ujumbe wa Twitter kwamba walikuwa na "mkutano mzuri".
 
Kwa nini Kim Kardashian anajihusisha na keshi hii?
Kwa mara ya kwanza Bi Kim Kardashian ambaye ni nyota wa kipindi cha maisha halisi cha televisheni nchini Marekani aliguswa na video fupi ya Bibi huyo juu ya kesi yake iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii.
Bi Kardashian West aliamua kumuomba wakili wake wa muda mrefu , Shawn Holley, kuiangalia upya kesi yake na akailipa timu ya mawakili wa Bi Johnson
 
Nyota huyo wa kipindi maarufu cha televisheni cha ....Keeping up with the kardashians , pia aliweza kushirikiana na Bwn. Kushner, mshauri wa ngazi ya juu wa rais Trump ambae amekuwa akishinikiza kufanyika kwa mageuzi wa magereza ya kitaifa.
Muswada wa Bwn. Kushner unaofahamika kama First Step Act, ambao umetengewa dola milioni $50 kwa ajili ya kusaidia kurekebisha tabia za wafungwa , ulipitishwana Bunge la wawakilishi nchini Marekani wiki iliyopita.
 
Kwa mujibu wa mabinti zake Johnson , mchakato huo umekwenda haraka kutokana na uhusika wa Bi Kardashian West.
Jumatano pia ni tarehe ya kuzaliwa ya Bi Johnson , ambayo Bi Kim Kardashian West aliikumbuka kupitia ujumbe wake wa Twitter alioutuma leo asubuhi.
 
Alice Marie Johnson ni nani?
Johnson alihukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela kisicho na uwezekano wa msamaha wowote mwaka 1996 kwa mara ya kwanza kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya ambayo hayakusababisha ghasia .
Alipatikana na hatia ya kutumiwa kama " chambo ", cha kusambaza ujumbe baina ya wauzaji na wanunuzi wa dawa za kulevya.
 
Anatimiza vigezo vyote vya msamaha kwa wafungwa chini ya mradi wa rais wa zamani wa Marekani ulioanzishwa mwaka 2014, lakini alikataliwa msamaha siku kadhaa tu kabla ya muhula wake kumalizika .
"Hii ni mara ya mwisho kuipa familia yangu shauku ya matarajio ya kuisikitisha ," Bi Johnson aliiambia BBC wakati huo.
Licha ya hilo, suala la kuingilia kati kwa Bi Kardashian West katika kesi hii linaonekana kuimarisha juhudi za kufunguliwa kwake.
 
Amy Povah, ambaye ni mmoja wa waasisi wa mradi wa msamaha kwa wafungwa unaofahamika kama CAN-DO ambae amekuwa akiendesha kampeni ya kufunguliwa kwa Bi johnson tangu mwaka 2014 , amesema kuwa amekwisha kusanya saini 70 kutoka kwa mashirika ambayo yanaunga mkono kuachiliwa kwake pamoja na barua ya kuunga mkono hatua hiyo kutoka kwa mkuu wa zamani wa gereza alimofungiwa Bi Johnston.
Nyaraka hizo zote zinaweza kuwasilishwa kwa rais Trump.
 
Kipi kitarajiwe?
" Binafsi nimekuwa nikimuona kama mtu wa kipekee ," amesema Bi Povah. "Si mtu mwenye machungu wala hasira , ni mtu anayekuonyesha matumaini."
Mchakato wa msamaha utategemea maamuzi ya rais , na haijafahamika hadi sasa ikiwa anapanga kutangaza uamuzi wake wakati Bi Kardashian West amemtembelea au la.
Wengi katika mitandao ya kijamii wamekosoa uhusika wa Bi Kardashian West kwa kujifanya mwanaharakati wa mageuzi ya magereza, wakisema kuwa kuna maelfu ya kesi zinazostahili kuchunguzwa kwa karibu , lakini mabinti zake Johnston bado wana matumaini kwamba kwamba kama familia walau hawataendelea kussubiri sana kabla ya kuachiliwa.
"Tunaomba msamaha katika kesi ya mama yetu … ili hatimae machungu tuliyonayo kama familia yamalizike ," Aliiamnbia BBC Bi Tretessa Johnson .
 
Mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah ataweza kushiriki katika michuano ya kombe la dunia , tafa lake limetangaza.
Daktari wa timu ya taifa hilo amesema kuwa matibabu ya kiungo huyo wa mashambulizi hayatachukua zaidi ya wiki tatu huku taifa lake likitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Uruguay mnamo tarehe 15 mwezi Juni.
Salah, 25, alikutana na daktari huyo pamoja na rais wa shirikisho la soka nchini Misri Hany Abu Rida nchini Uhispania siku ya Jumatano.
Shirikisho hilo baadaye lilituma ujumbe wa Twitter likisema: Baada ya kukutana na Abu Rida pamoja na daktari wa timu ya taifa nchini Uhispania leo, Shirikisho la soka linathibitisha kuwa Salah atashiriki katika kombe la dunia, Mungu akipenda.
 
Back
Top Bottom