Kipi kitarajiwe?
" Binafsi nimekuwa nikimuona kama mtu wa kipekee ," amesema Bi Povah. "Si mtu mwenye machungu wala hasira , ni mtu anayekuonyesha matumaini."
Mchakato wa msamaha utategemea maamuzi ya rais , na haijafahamika hadi sasa ikiwa anapanga kutangaza uamuzi wake wakati Bi Kardashian West amemtembelea au la.
Wengi katika mitandao ya kijamii wamekosoa uhusika wa Bi Kardashian West kwa kujifanya mwanaharakati wa mageuzi ya magereza, wakisema kuwa kuna maelfu ya kesi zinazostahili kuchunguzwa kwa karibu , lakini mabinti zake Johnston bado wana matumaini kwamba kwamba kama familia walau hawataendelea kussubiri sana kabla ya kuachiliwa.
"Tunaomba msamaha katika kesi ya mama yetu … ili hatimae machungu tuliyonayo kama familia yamalizike ," Aliiamnbia BBC Bi Tretessa Johnson .