Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.
Alisema mnamo mwezi Januari kwamba ataondoka katika klabu hiyo atakapohisi kwamba hana la ziada kuisaidia timu hiyo.
Hatahivyo , tangazo linaonekana kuwashangaza wengi kwa kuwa linajiri siku chache tu baada ya Real kuishinda Liverpool 3-1 katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya
"Hii ni klabu ambayo imeshinda mataji 13 ya Ulaya , kwa hivyo nafurahia kuwa miongoni mwa historia yake'', alisema baada ya ushindi mjini kiev.
Tutafikiria kuhusu kile tulichofanikiwa kufanya. Tufurahie. Huu ndio wakati muhimu zaidi.
 
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino amehusishwa na klabu ya Real siku za hapo nyuma. Raia huyo wa Argentina hatahivyo aliweka kandarasi ya miaka mitano na Spurs wiki iliopita.
Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri huenda pia akahusishwa kujaza pengo hilo , huku Arsene Wenger akitaka kuendelea na ukufunzi baada ya kuondoka Arsenal baada ya miaka 22.
Mkufunzi raia wa Itali Maurizio Sorri wa klabu ya Napoli pia anapatikana. Uamuzi wa ni nani atakayesimamia Real Madrid utatolewa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez.
Aliandamana na Zidane katika mkutano huo na vyombo vya habari na kusema kuwa angependelea kumshinikiza mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 1998 kusalia katika klabu hiyo.
 
Huu ni uamuzi ambao hatukuutarajia. Zidane aliniambia kuhusu uamuzi wake jana'', aliongezea Perez.
Kuondoka kwa Zidane kunajiri baada ya Gareth Bale na Christiano Ronaldo kufichua kwamba wanafikiria hatma yao katika klabu hiyo.
Mshambuliaji wa Wales, Bale hakufurahia kushiriki katika mechi ya fainali ya vilabu bingwa dhidi ya Liverpool kama mchezaji wa ziada huku Ronaldo akisema baada ya mechi hio kwamba atafanya uamuzi kuhusu hatma yake.
Alipoulizwa iwapo uamuzi wake unatokana na Ronaldo, Zidane alisema: Real inatafuta meneja wake wa tano katika kipindi cha miaka mitano.
 
Nahodha wa Peru Paolo Guerrero anaweza kucheza kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi, jopo la mahakama nchini uswizi limeamua.
Mahakama hiyo ilikubaliana kuondoa kwa muda marufuku ya kutocheza miezi 14 ambayo ilikuwa imetolewa dhidi ya mchezaji huyo na Mahakama ya kutatua Mizozo ya Kimichezo (CAS).
Mahakama hiyo ilichukua hatua hiyo huku ikiendelea kusikiza rufaa ya mshambuliaji huyo wa miaka 34.
Manahodha wa timu zilizopangwa kucheza na Peru katika Kundi C Australia, Denmark na Ufaransa walikuwa wameliandikia barua Shirikisho la Soka Dunia Fifa kuwataka wamruhusu mchezaji huyo kucheza.
Guerrero, ambaye alipatikana na kosa la kutumia kokeni Oktoba, anasema alijipata amekunywa dawa hizo akinywa chai.
Anatumikia marufuku ya miezi 14.
 
Kupitia barua kwa Fifa, manahodha hao watatu waliomba kuwe na "kusitishwa kwa muda" kwa marufuku yake ndipo aweze kuchezea Peru nchini Urusi.
Kokeni kwenye chai
Guerrero, 34, alipatikana ametumia kokeini wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Argentina mnamo 6 Oktoba na akapigwa marufuku ya miezi 12 awali.
Marufuku yake ilipunguzwa hadi miezi sita na kamati ya rufaa ya Fifa lakini shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni (Wada) lilikakata rufaa uamuzi huo kwenye Mahakama ya Mizozo ya Kimichezo (Cas) ambayo ilimpiga marufuku ya miezi 14.
 
Mahakama nchini uswizi sasa imeamua kuwa hatua ya kuongeza marufuku hiyo haikuwa ya haki na imeondoa utekelezwaji wa marufuku hiyo kwa sasa, hatiua inayomwezesha Guerrero kucheza katika michuano hiyo itakayoanza mnamo 14 Juni nchini Urusi.
 
ZIDANE ilikuwa ni lazima aondoke kwa sababu:-

1.Alitofautiana kimsimamo na kimtazamo na Dikteta wa Madrid.

2.Dikteta Hakupendezwaa na Zizzou kutobeba Copa Del Rey na La Liga.

3.Zizzou kumtetea Navas asiuzwe dikteta alichukia.

4.Dikteta alitaka kusajili players ambao Zizzou hapendezwi nao.Aliowataka Zizzou, Dikteta aliwakataa.

5.Dikteta huwa hajui ugumu wa soka wa changamoto zake, yeye anataka ushindi kila mechi na kutwaa kila kombe.

6.Dikteta alitaka Galacticos kama ile ya miaka ya 2000's-2004 na mchezo kama wa Arsenal moja moja za kufikia.

7.Zizzou hapendi kuendeshwa au kupelekeshwa.

8.Zizzou amependa kuonda kabla hajafukuzwa.

9.Zizzou amependa kuondoka kabla hajachokwa wala kuharibu record yake na kabla hajachuja.

10.Dikteta hakupenda ZIZZOU kumtetea Benzema.

11.Kujifungia vyumbani masaa zaidi ya mawili kwa Zizzou & Players wote kulimuudhi sana dikteta.

12.DIKTETA ANAVUNGA KWA WAANDISHI, MOYO WAKE UNATABASAMU KWA NDANI KWA ZIZZOU KUONDOKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…