Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini Mourinho anataka kutumia pesa hiyo kwenye kusajili wachezaji wengine makini, ambao atawapata wengi kuliko kumsajili Bale mmoja. Kocha huyo Mreno kwa sasa akili yake haijatulia kabisa hadi hapo atakapowanasa viungo Fred na Sergej Milinkovic-Savic, ambao amekuwa akiwawinda kwa muda mrefu. Kiungo Fred, anayekipiga kwenye kikosi cha Shakhtar Donetsk amesema anasubiri hadi Kombe la Dunia limalizike ndipo atakapoamua hatima yake na kwamba saini yake inaweza kupatikana kwa Pauni 35 milioni tu.
 
Real Madrid ametoa mkono wa kwaheri kwa Zinedine Zidane Alhamis, wakati Mfaransa huyo akiwa katika kilele chake cha mafanikio ya ukocha.
Zidane amepata mafanikio makubwa katika siku zake 878, alizokuwa katika klabu hiyo akiwa ametwaa mataji tisa yakiwemo mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Uamuzi wake wa kustaafu umekuja siku sita baada ya kunyakuwa taji kubwa barani Ulaya, Pia Zidane hajawahi kutolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa tangu alipokuwa kocha wa Real Madrid.
 
Mfaransa huyo ameweka rekodi ya kushinda fainali nane alizocheza kwa nyakati tofauti, akiwafunga Atletico, Juventus na Liverpool katika Ligi ya Mabingwa, katika Kombe la Dunia la Klabu la Fifa amezifunga Kashima na Gremio, pia alizifunga Sevilla na Manchester United katika UEFA Super Cup pamoja na Barcelona katika mchezo wa Supercopa de Espana.
 
Mataji yake mengi aliyochukua ni LaLiga taji alilochukua msimu wa 2016/17, baada ya Real Madrid kusubili kwa miaka mitano.
Akiwa na makombe tisa, Zidane anakuwa kocha wa pili mwenye mafanikio zaidi katika klabu hiyo akizidiwa na Miguel Munoz mwenye makombe 14.
Zidane msimu uliopita alishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Fifa.
Taji pekee aliloshindwa kunyakuwa ni Kombe la Mfalme, ambalo Barcelona imelitawala zaidi.
 
Baada ya uamuzi wa kocha wa Real Madrid kutangaza jana Alhamisi kuhusu mpango wake wa kuachana na Real Madrid, nyota wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo ametuma ujumbe mzito Istagram akimshukuru kwa kuendelea kumpa makali kikosini hapo.
Mreno huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Istagram akisema “Ninajivunia kuwa mchezaji wako, kunifanya niheshimike, nakushukuru sana.”
 
Back
Top Bottom