Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya Ronaldo kuandika ujumbe huo, mashabiki takribani milioni sita ‘walicomment’ kwenye ukurasa huo wa Istagram, huku wengi wao wakimsihi Zidane asiondeoke.
Zidane alitangaza kujiuzulu jana Alhamisi akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
 
NDIYO hivyo. Derby County imemteua Frank Lampard kuwa kocha wake mpya na kumsainisha mkataba wa miaka mitatu.

Derby imekuwa ikisaka kocha mpya tangu Gary Rowett alipoondoka kwenda Stoke City na Lampard, kiungo wa zamani wa Chelsea na England amekuwa kwenye mazungumzo na timu hiyo kwa siku chache za karibuni na kupewa kibarua hicho.
 
Siku zote nilihitaji kuwa kocha kwenye klabu yenye historia na utamaduni mkubwa kama ilivyo kwa Derby County, hivyo ni fursa ya kipekee. Nimetumia muda mwingi kuzungumza majukumu yangu na mipango ya mwenyekiti na wajumbe wa bodi wa klabu,” alisema Lampard.“Tunataka kuendelea pale ilipomaliza timu msimu uliopita ambapo ilishika namba sita kwenye chambionship, huku kwa muda huohuo tukijaribu kupandisha vijana mahiri kutoka kwenye akademia. Hii ni kazi yake ya kwanza, lakini nimebahatika kufanya kazi na makocha bora kabisa, hivyo nina uhakika wa kufanya vyema kwenye timu yangu.”

Lampard alistaafu soka mwaka 2016 akiwa na klabu ya New York City FC.
 
JOSE Mourinho amewaambia mabosi wake huko Manchester United wasiivuruge kabisa bajeti yake kwa kumsajili Gareth Bale kwa Pauni 200 milioni.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo ya Old Trafford, Ed Woodward ameonekana kuwa na mpango wa kumnasa staa huyo wa Real Madrid ikiwa moja ya mipango ya Man United katika kusajili mastaa wenye majina katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya.
 
Lakini Mourinho anataka kutumia pesa hiyo kwenye kusajili wachezaji wengine makini, ambao atawapata wengi kuliko kumsajili Bale mmoja. Kocha huyo Mreno kwa sasa akili yake haijatulia kabisa hadi hapo atakapowanasa viungo Fred na Sergej Milinkovic-Savic, ambao amekuwa akiwawinda kwa muda mrefu. Kiungo Fred, anayekipiga kwenye kikosi cha Shakhtar Donetsk amesema anasubiri hadi Kombe la Dunia limalizike ndipo atakapoamua hatima yake na kwamba saini yake inaweza kupatikana kwa Pauni 35 milioni tu.
 
Mchezaji mwingine anayemsaka ni Sergej na anaamini staa huyo wa Serbia anastahili kwenda kwenye kikosi chake, huku akiwindwa pia na timu nyingine kibao zikiwamo Juventus na Manchester City.
 
ARSENE Wenger anasema inaboa kukaa bila ya kazi na hivyo ameziita timu vigogo kwenda mezani kwake kumpa dili la maana la kufanyakazi ili kuondokana na upweke unaomkabili kwa sasa.

Baada ya kudumu kwenye kikodi cha Arsenal kwa miaka 22, Wenger aliachia ngazi mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi karibuni, lakini kwa sasa ameshachoka kutokana na kitendo cha kutokuwa na kazi ya kufanya.
 
Wenger, 68, alizungumzia mpango wa kujipa mapumziko mafupi baada ya kung’oka kwenye ukocha wa kuinoa Arsenal, lakini kutokana na upweke wa kuwa mbali na soka ameziambia klabu vigogo kumpa dili la kazi mpya.

“Mimi si mtu wa kupenda kufurahia maisha huko kwenye fukwe, hivyo nawaonea sana wivu marafiki zangu wanaoweza kuishi maisha hayo,” alisema Wenger.
 
Kwa haraka sana imeshaniboa, kwa sababu hii ni kama ulevi ambao nimejizoesha. Ni ulevi niliojizoesha ambao unahitaji kuishi nao muda wote.”

Wenger alisema kwamba klabu yake mpya itahitaji kuwa na muunganiko spesho baina ya wachezaji na mashabiki. Kwenye nafasi yake ya Arsenal alikotoka kwa sasa timu hiyo imemtangaza Unai Emery kuwa kocha wao mpya na sasa ameanza na mipango ya kukisuka upya kikosi hicho cha Emirates ikiwa pamoja na kusajili wakali wapya.
 
Kwa haraka sana imeshaniboa, kwa sababu hii ni kama ulevi ambao nimejizoesha. Ni ulevi niliojizoesha ambao unahitaji kuishi nao muda wote.”

Wenger alisema kwamba klabu yake mpya itahitaji kuwa na muunganiko spesho baina ya wachezaji na mashabiki. Kwenye nafasi yake ya Arsenal alikotoka kwa sasa timu hiyo imemtangaza Unai Emery kuwa kocha wao mpya na sasa ameanza na mipango ya kukisuka upya kikosi hicho cha Emirates ikiwa pamoja na kusajili wakali wapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…